Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kudadeki ! MSHAHARA ungekuwa unapigika ROBA ningeukwida roho walakhi!:-(

>> Tuesday, January 11, 2011





Ndio,...
....MSHAHARA ni moja ya sababu kuna mpaka NESI na DAKTARI mahospitalini ambao wako kwa ajili ya mshahara tu na HAWAPENDI wagonjwa!:-(




MSHAHARA,....
.... ni moja ya sababu kuna mpaka MBUNGE katika BUNGE la TANZANIA au hata KENYA  ambaye ukiondoa MSHAHARA anaweza kuacha UBUNGE hata kwa kujifanya ni MGONJWA.:-(





Swali:
  • Kwani unafikiri ni watu wangapi uwakutao MAKAZINI ambao  kifanyacho wawepo hapo ni MSHAHARA tu?

  • Lakini si unakumbuka labda mtoto mzuri mgawaji   udhaniaye anagawa ili kukidhi mahitaji kwa kuwa mshahara mdogo bado ataendelea kugawa  tu kama ugawaji ni tabia yake hata akilundikiwa bonge la mshahara?



Kudadeki  MSHAHARA,....
.....maana LEO wafanya mpaka kuna asiyependa kinyesi kufanya kazi za usafi wa choo cha stendi chenye mavi pembeni ya shimo UBUNGO au tu stendi ya mabasi MOROGORO!

DUH!:-(
'

WAZO limenishinda!:-(
Ila ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala USIKONDE!:-(

Hebu Mossy Suleiman na  Zanzibar STARS asemenaye kuwa -Usione soo! sema nae



Au turudi tu Durban, Afrika KUSINI ili tena Proffessor,Oskido na Dj Tira watupe RIDHIMU  ya siku ya leo katika kitu -Jezebel

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 11:55 am  

Mkuu haki baada ya wajibu ni muhimu!

emu-three 2:00 pm  

Mshahara weee! hata kama mtu hana anachofanya ofini na mwenzake anapigika kufa na kupona, bado ikifikia mshahara hasemi mpe yule zaidi kwasababu kapigika sana kliko mimi...mshahara weeee, we acha tu

chib 6:04 pm  

Napinga hiyo ya madokta na manesi :-)

Rachel Siwa 7:57 pm  

Baadhi ya watu wanaenda kazini huku sura wamekunja! baadhi ya manesi bongo ukimwita nesi naomba msaada anakuona msumbufu je yupo hapo kwanini ni MSHAHARA TUUUUU!!!!!!!!!

nyahbingi worrior. 8:45 am  

mkuu Simon,kwema,nimepita kusoma mambo yako mkuu,ila kurasa imebadilika mkuu,au?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP