Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKIRITIMBA kitandani!:-(

>> Wednesday, January 12, 2011

Kitanda!


Ndoto haziishi KITANDANI!
Mipango ihitajio utoke KITANDANI,...
.....hata isiyowezekana yawezaonekana kama inaweza  kutendeka  wakati uiwaziapo ni KITANDANI!

 Na wengine huzaliwa KITANDANI!
Na ni mahali maarufu sana KUUGULIA pale KITANDANI!:-(
Na kuna watu wengi hufia hapohapo  KITANDANI!



Na kuna watu wadaio kuwa ajiitaye MHESHIMIWA kwa kawaida hujamba kwa uhuru kistarehe zaidi kuliko akiwa chooni  akiwa pekee KITANDANI!:-(

Na ngono na ulawiti yasemekana hufanyiwa sana tu  zaidi KITANDANI

Na nawaza tu  ni mangapi leo hapa DUNIANI yamefanywa hata bila MTU kuondoka KITANDANI!:-(

Swali:

  • Si inakumbukwa lakini MENGI hata yawaziwayo KITANDANI ukitaka kuyafanikisha kivitendo itabidi UTOKE KITANDANI?


Ndio,....
....labda tutoke KITANDANI ,...
.... ili kwa vitendo tuelekee kwenye MAENDELEO  tuyawazayo KITANDANI!:-(



Swali zaidi:
  • SI labda kuna watu mpaka wako mashuleni na MAOFISINI lakini ubongo wao bado umelala nyumbani pale KITANDANI?


Kitandaaaaaaaaaaaaaa,....
....pole na shughuli ingawa labda ni MEZA ya jikoni ikatwayokatwayo sana na VISU katika shughuli hata zile za kutengeneza KACHUMBARI!:-(

NI WAZO TU HILI mkweche  MHESHIMIWA!:-(

Tubadili kwa kusikiliza majibishano ya WANAMUZIKI waliowahi kuwa kikundi kimoja wakijibishana kistaarabu baada ya kutengana ,...
...tuanze na FAZE katika-Letter to my Brother



Halafu 2face Idibia ajibu katika-See me so



2Face Idibia hebu abadili kwa kurudia tena -African Queen



Au WATU WAZIMA  wenye muziki wa kiutu uzima Onyeka Onwenu na King Sunny Ade waingilie kati na-Wait for me

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:57 pm  

kama shghuli zenyewe ndio hivyo Kaaazi kwelikweli:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP