Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MAPENZI - baada ya kuanza TENA kutumia AKILI na kuvaa tena chupi!:-(

>> Monday, January 10, 2011

Yasemekana MAPENZI ni kama aina ya UKICHAA,...
... ndio maana aliyependa KIKWELI KUTOKA MOYONI kuna wamshuhudiao walalamikao,.....
....kuwa HASIKII , haonyeki na  wala HAAMBILIKI,....
...kwa kuwa KAPENDA,.....
.... na aliyependa yasemekana  huwa hatumii sana AKILI!:-(


Swali:
  • UNabisha?

Na kuna uwezekano MTU apendaye KUTOKA MOYONI huwa  hachagui wa KUMPENDA,...
.... na kama wewe ulichagua unayempenda ,...
....basi wewe katika MAPENZI yako ulitumia AKILI,....
..... na mapenzi yoyote yaliyoanza kwa kutumia AKILI,.....
..... labda  ukiyachunguza UNDANI utagundua labda HAYAKUTOKA MOYONI au angalau  ni kweli hayana misingi yake MOYONI;...
... na  kuna ambayo utastukia PIA  kwa kuwa  HAYATOKI MOYONI ,...
....misingi yake iko kwenye POCHI au UJIKO TU wa mtu  utokanao na MTU kufikiria hivi watu WENGINE WANAFIKIRIA NINI ,....
.....na wala hata sio angalau MISINGI ILIYOZOELEKA ile ya mvuto wa chini ya kitovu  cha ALENGESHWAYE PENZI  pale katikati ya miguu  au tu mvuto wa TAKO na nyonyo kama baadhi walivyozoea KUSINGIZIA PENZI  wakati wanajikuta wanarudirudi kwa TOTO JINGA ila zuri .:-(


Swali:
  • AU?


Ndio,...
... kama unamajibu kibao kwanini unapenda MTU tokea mwanzo wa penzi,...
.....labda MAPENZI yako asili yake sio MOYONI:-(


Swali zaidi kiduchu:
  •  Si unajua aliyependa KWA DHATI KUTOKA MOYONI na sio kutoka mkao wa CHUNA BUZI  akiwekwa kikao  na kuulizwa kwanini anampenda MTU ni kawaida kutokuwa na jibu kwa kuwa mengi kuhusu huyo mtu  aliyempenda hajayafikiria?
  • Kwani hujui kuna watu wengi WENYE AKILI LUKUKI TU  ni baada ya kuvua chupi ndio huanza kutumia akili na kufikiria labda kilichofanyiaka ni kitendo cha kijinga na kujiuliza sijui nimepata MIMBA?


Ndio,...
... wengi wamepata MIMBA, gono mpaka  UKIMWI,....
.... halafu ndio wakaanza kutumia AKILI,...
.... kama tu ambao mpaka WALIPOOA na KUOLEWA ndio wakaanza kutumia akili na kuanza kuelewa ni kwanini kuna watu WALIKUWA WANAWAONYA kuwa walikojiingiza ni kule katika KUCHEZEA moto,....
.... ingawa katika muda huo WANAZINDUKA KATIKA USINGIZI WA AKILI KUTOKANA NA UTAMU WA PENZI na kuanza kutumia AKILI ,....
....ni wakati WANAUNGUA  TAYARI na mchuma ndio ushatoka huo.:-(


Swali:

  • Sasa wakati unajua mapenzi ni KIZUNGUZUNGU utalaumu kweli   ALIYEPENDA kwa dhati kutoka MOYONI  wakati CHA MOTO ANAKIONA wakati unajua APENDAYE kwa dhati kutoka MOYONI labda pendo lake ndio la KWELI  hasa ukizingatia angepenga kiuongouongo kwa kutumia AKILINI labda angechagua KIBOSILE na sio dereva wa KIBOSILE awezaye shughuli za nipe nikupe vyema zaidi  kwa staili za tukunyema kwa kuwa hana KITAMBI  lakini KIBOSILE mwenye kitambi ndiye MWENYE POCHI lenye za kutosha pesa ambacho ndicho kitu muhimu kwa wengi  wahusuduo maisha SHALLOW aka YA KIUUZA SURA  yenye chati  kibinadamu hasa wale wapendao ANASA?

MAPENZI kirahisi yanaweza vua MTU chupi,...
..... na baada ya MTU  kuvaa chupi  na kuanza kutumia tena AKILI,....
.....mtu ANAWEZA KUSTUKIA PIA  mapenzi yaliyoanzia MOYONI  bila kutumia akili ili yadumu,....
.... kwa bahati mbaya  nayo yatahitaji tu  MTU atumie AKILI kama nia nikuyatunza yadumu ,...
... na kwa bahati mbaya wakati huo mtu huwa KASHAONJWA tayari  na malighafi sio bikira tena!:-(





TOPIKI IMENISHINDA!:-(
Na MKUU kumbuka kuwa nawaza tu hapa hata kama ni kwa stahili ISIYOHESHIMIWA!:-(
Na samahani ngojea niyatukane MAPENZI kidogo;...
...Mapenzi SHENZI wee MAPENZI, lione vile  meno kama kijambio cha kuku!:-(


Na NIMEACHA WAZO MHESHIMIWA!:-(



Hebu Lopango ya BANKA warudishe ustaarabu hapa kijiweni kwa ndude Nipo na KONGO.....Samahani jiwe hili ni -MPO NA KONGO




Lopango ya Banka waendelee na kitu  - Bifuku Mitano



Na au tu AWILO Longomba aingilie kati shughuli tena kwa-Coupe bibamba




Bado nipo....!:-(















































1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:59 pm  

Mapenzi:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP