Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo katika kufikia uamuzi UFISADI ni dhambi, ULAWITI ni dhambi lakini UZINZI na ULEVI sio dhambi sana kama tu vile KUDOKOA MBOGA!:-(

>> Thursday, January 20, 2011

BINADAMU anamchezo wa kuchagua nini ni DHAMBI,...
....ndio maana anayefanya UZINZI  hata wakutamani MTU wa WENZIYE  ambao wengine wanauona na kutafsiri  ni dhambi kama dhambi nyingine,....
.... anaweza akawa naye ananyoshea vidole MAFISADI  wale WEZI , wauaji ,.....
.....kwa kuwa yeye wakati huo aonacho ni DHAMBI tu za wengine!:-(

Swali:
  • Si umestukia kuwa MUUAJI anaweza akawa anachukia kweli WAZINZI ?
  • Na si unajua KUNA wauaji wauao kwa UFISADI tu usababishao HOSPITALINI hakuna DAWA?

Ndio,...
...labda wakati mtu anastukia zaidi wanavyokosea watu wengine na kuchukizwa sana na DHAMBI za wengine,....
.... si vibaya akijichunguza  ni dhambi gani anairuka yeye mwenyewe  aifanyayo hata wakati huohuo ananyoshea vidole watu wengine,.....

....kwa kuwa labda KIBINADAMU  kuna  DHAMBI inafungiwa tu macho wakati mwingine kwa kuwa ni tamu au imezoeleka na vionekanavyo vibaya ni vile tu vya WENGINE.:-(


Swali:

  • AU?

Ndio,...
.... labda kuna kitu KUFIKIA UAMUZI mpaka katika ni nini LEO kwa mtu ni DHAMBI SANA,....
.... au si dhambi sana  hata kwa vigezo tu kuwa uliifanyia migombani hata bila kuguna  na hakuna aliyestukia.:-(


Nawaza tu hapa MHESHIMIWA na wala usikonde!:-(




Hebu K. Kilonzo arudie-Wakumbuke Wazazi




Au Luther Vandross abadili mkao kwa kuuliza tu tena-Can Heaven Wait



Halafu sijui kwanini lakini hebu na  ASWAD ngojea tu nao wadinye tu -Roots Rocking

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:16 pm  

Mtakatifu umenikumbusha mbali sana enzi zile mwaka 47 kudokoa mboga:-) na asante kwa mziki hasa kibao hicho cha kwanza tusiwasahau wazazi.

Simon Kitururu 5:43 pm  

@Dada Yasinta: Tuko pamoja Mpenzi!

Rachel Siwa 7:19 pm  

Kaka Kitururu Jambazi anachukia walevi, walevi wanachukia majambazi!!!!!!muongo anachukia msengenyaji mmmmh dhambi dhambi tuu hakuna kubwa wala ndogo!

kaka leo mbona umewaza sanaaaaa?

Simon Kitururu 7:35 pm  

@Swahili na WASWAHILI: Niko tu mawazoni DADA yangu RACHEL!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP