Jinsi ya kukabili KUJIJUA!
>> Monday, January 03, 2011
Katika safari ya MTU ya kujijua,......
...... mtu anaweza mpaka kustukia mengi DHAIFU yasiyo rahisi kukiri ndiyo sehemu ya yeye.:-(
Swali:
- SI kunauwezekano katika kujijua kwa MHESHIMIWA MWIZI, mwizi anaweza kupata taabu kukubali UKWELI kuwa yeye ni MWIZI na afanyacho ni wizi mtupu hata kama ni wa KALAMU?
Ila,....
.....labda kwa KUJIJUA kwa mwizi kuwa afanyacho ni WIZI,.....
....kunaweza kuwa ni msaada kwa MWIZI katika kusaidia mwizi kuridhika na wizi wake kitu kiwezacho kumsaidia KUIBA kwa starehe,......
....kwa kuwa angalau wizi utafanywa wakati roho imetulia.:-(
NI wazo tu hili!
Naendelea kuwaza.....Kwa kuwa ni JUMATATU hebu tukumbushwe wikiend na Afro 70 Band katika jiwe-Wikiendi
Au tu ngojea TATUNANE waingilie shughuli kwa-Msewe
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh! Bro mawazo yako ni ya ukweli na yanazidi kunifanya nifikirie mambo kwa undani zaidi,unaweza ukawa unajua una udhaifu fulani lakini kukubali kuwa ni udhaifu ikawa ngumu lakini ukiwa unauona kwa mtu mwingine ikawa ni kero kwako.Heri ya mwaka mpya!
Kweli mkuu hata mlevi hakubali kuitwa mlevi, kama alivyo fisadi asivyokubali kuitwa fisadi. Ni ubinadamu kuwa hakuna anayependa kuitwa `wasivyopenda watu' hata kama ni `sifa', lakini kwa vile jamii haikubali kuwa ni sifa basi waogopa kuitwa hivyo.
Wakumbuka wapigania uhuru walikuwa wakiitwa majina mabaya, ambayo baadaye yaligeuka kuwa sifa! Nimewaza tu mkuu, tupo pamoja
@Ney: Heri ya Mwaka mpya Dada yangu!
@M3: Nakubali kabisa ulilosema Mkuu!
Post a Comment