Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA , kuna mambo ni ya KIBINADAMU na MUNGU anasingiziwa tu!:-(

>> Tuesday, January 04, 2011

NDIO,...
......kwa waaminio MUNGU bado  BINADAMU kapewa akili,.....
.... na kuna mambo LABDA tishika na hoja za BINADAMU hasa kama mtoa hoja anakazia sana mchango wa MUNGU,....
..... hasa  ukizingatia liongelewalo ni la BINADAMU MWENYEWE kutumia akili tu!:-(

Swali:

  •  Si umestukia  kuwa kuna mambo BINADAMU huweza tu  hata kwa kutumia akili tu ndio maana UKIMWI hauishi na pia MAFISADI labda ndio wafanikishao zaidi angalau KUIBA  katika kundi la wananchi?
  • Si unajua katika WACHANGIA HOJA  wapo tu na ambao  hutumia tu jina la MUNGU kutaka tu hoja zao za KIVIVU zisizo na uhusiano na MUNGU zipewe tu UZITO kama hoja HASA na wale wasikilizaji waogopao MUNGU?

  • Na si hata kwa mcha MUNGU auguaye MALARIA na anajua kwa kutumia dawa ya MALARIA ya MUARUBAINI atapona  labda  ingawa MUNGU anaponya bado ni busara kutumia dawa pia na sio kuegemea MAOMBI tu?


Ndio,.....
.....ingawa  naelewa ni KWANINI watu wenye imani zao huona ni busara kumtanguliza MUNGU katika kila hoja mpaka zile za kutongoza hasa kama atongozwaye ni mwenye imani KIDINI ila siku hiyo kaudhaifu KAKIBINADAMU  kamemuingia kwa kuwa ukame umezidi,....
..... lakini LABDA sio mapenzi ya MUNGU,....
...... kwa mwenye uwezo wa kutumia  akili KUTOTUMIA AKILI kukabiliana na ya DUNIA   kwa KUZEMBEA,......
.... na kuendeleza UZEMBE kwa kisingizio kinachorembwa tu na hoja zisingiziazo MAPENZI ya MUNGU dangachee.:-(

Swali:

  • SI inakumbukwa kuwa TALANTA ya mtu inaweza isizae kama MWENYE talanta haichezei ili ipate mimba?

Kuhusu TALANTA kwa wenye BIBLIA Soma Mathayo 25:14-19.


Na hili ni WAZO TU MKUU!:-(

Na moja kwa moja tupate SINDIMBA kutoka ARUSHA kwa kikosi kamili cha MS Ngoma Troupe


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP