Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mazingira ni SHULE na kuna ujifunzacho tu kutokana na unapokulia!:-(

>> Thursday, January 27, 2011

Ndio,....
.... ukikulia KIJIJINI  kuna vitu tu utakuwa unajua zaidi ya waliokulia MJINI,....
.... kwa kuwa WATOTO wa mjini mazingira yao yanakawaida ya kubobea katika vitu vingine!:-(


Swali:
  • SI unajua watoto waliokulia mazingira yenye wasomi yasemekana kuna mambo huyajua hata bila kwenda kusomea kwenye ziitwazo SHULE?

Ndio,...
.... mazingira ni shule na MTU akikulia mazingira yaliyojaa MALAYA anaweza kujikuta anajua umalaya hata kama hatauita ni umalaya  HASA kwa kuwa kwa huyo mtu itakuwa tu ni MAISHA YA KAWAIDA na ni siku tu nyingine imepita.:-(

Swali:
  • Unabisha?


Ndio,...
..... labda WATOTO wa mjini kutokana na mazingira yao  kuna MAMBO shule yao ndogo,...
.... ukilinganisha na TOTOZ za kijijini!:-(

NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA!:-(


Hebu Asylum wabadili kwa-World's a ghetto






Au tu hebu DONNA SUMMER aturudishe miaka ya sabini tena kwa-I feel love

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 9:35 am  

Kwa hiyo hivi da mija ningekulia katika mazingira ya MASHOGA inawezekana nami ningekuwa si riziki au labda ningekuwa mtaalamu wa kitengo hicho...Bonge ya somo.

Kitururu uwe makini na wanao wapi unawakuzia.

Yasinta Ngonyani 1:30 pm  

Mija utadhani ulisema ngoja nimuwahi Yasinta kwa hayo ulosema.
Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na hufutisha jinsi wazazi/walezi wafanyavyo na kama tujuavyo watoto ni wazuri sana kwa kuiga.Hakika hili ni darasa kabisa....

emu-three 2:28 pm  

Wanasema ukikaa kwenye choo kinachonuka, utanuka mavi na ukikaa kwenye uturi utanukia uzuri...mkuu upo hapo!

Simon Kitururu 2:53 pm  

@Da Mija : LABDA! Si nasikia kuna wanawake kwa kuwa wanaamini tu ni kazi ya mwanamke kumkubalia mwanaume wanakubali tu kila mme wao akihitaji chakula cha usiku hata kama inauma kwa kuwa mazingira waliokulia katika jamii kumkatalia mme wamefundwa ni kosa ambalo wanaweza hata kuachika?

Naamini umakini ni muhimu na ukiwa makini unaweza bado kukontroo jinsi wanao wanavyoangalia na kujifunza kutoka katika mazingira na kama hauko makini hata kama weye ni ASKOFU au SHEKHE waweza shangaa watoto wako MAJAMBAZI au tu viruka njia na unabaki kushangaa mbona nyumbani tunaswali ila ZE TOTO hazijajifunza kitu kutoka katika SWALAZ!

@YASINTA: Kwani wewe unafikiri ni kwa muda gani uko na watoto wako katika maisha ya siku hizi? Hudhani kunauwezekano ni watu wengine walioko kwenye mazingira yako labda ndio wakutanao na watoto wako labda hata kuliko weye MZAZI ambaye masaa kibao uko kazini na labda jioni watoto wakiwepo na wewe wewe uko hoi kutokana na shughuli za siku?


@M3:

Na kwa bahati mbaya ukikaa muda mrefu kwenye choo mpaka ukaambukizwa harufu ya choo, pua nayo huzoea na kufanya usistukie unanuka choo wakati unaendelea na shughuli zako nje ya choo.:-(

Yasinta Ngonyani 4:49 pm  

Nakubaliana nawe ni kweli ni muda mchache sana nakuwa na wanangu na watu wanaokuwa nao ni WALIMU WAO. Ndio maana kuna wakati inabidi kutafuta muda na kuwa nao na hiyo nayo inakuwa kasheshe..Ahsante kaka Simon kwa kunikumbusha hili si unaona hata hilo nasahau..mweee :- nanukuu "labda jioni watoto wakiwepo na wewe wewe uko hoi kutokana na shughuli za siku?" Si utani na unataka kwenda kulala moja kwa moja.

Jeff Msangi 6:52 pm  

Labda niongeze kwamba mazingira ni shule,darasa,mwalimu mkuu,kiranja mkuu.

Lakini,je upo uwezekano wa kubadili tabia ya mtu ambayo alijifunza au kujishtukia anayo kutokana na mazingira aliyokulia?Nadhani inawezekana,japo kwa shida na ugumu wa aina yake.Wanaita Rehabilitation..au sio?

Simon Kitururu 3:25 am  

@Jeff: Ndio uwezekano upo na nahisi ni reverse tu ya ilivyo mtu awezavyo kuharibika baadaye.

Na si nasikia hata MAFISADI wengi ufisadi ni mambo walijulia tu mbele ya safari ya kukua maofisini UKUBWANI?

Na hisi hiyo ni aina tu ya Rehabilitation kinamna ibadiliyo toto zuri kuwa KUBWA fisadi ukubwani hata kama utotoni lilikuwa toto la MKULIMA .:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP