Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

PEREMENDE TAMUTAMU na UKWAJU CHACHU katika MTU yuleyule hata nikiwa na HAMU ya KUBISHA!

>> Monday, January 17, 2011

Afikiriwavyo MTU yuleyule  VILE,...
...... ni mchanganyiko wa alivyo YULE na alivyo amfikiriaye  YULE  vile ,...
.... bila kusahau ya mpaka  YALIYOPO katika sehemu kimazingira ambayo yanatanua KILE kistukiwachokirahisi  VILE  ambacho ,...


...aonekanaye , asikilizwaye au tu yaliyopo  katika MAZINGIRA yafanyayo KITU kitafsirishe  zaidi KIAINA baadhi yayafikiriwayo ndiyo YATAFSIRIYO  NDIVYO yaliyopo ndani ya MTU ambayo ndiyo   yafanyayo iaminike ndivyo MTU alivyo!:-(



Swali:
  • SI unajua kuna ukutananaye MLEVI ustukiayo wakati kalewa labda wala sio yale ambayo ungestukia kama ungekutananaye wakati hajalewa na aongeleacho  ni KEMIA na BAOLOJIA  au tu DINI na SIASA  kama upendavyo?
  • Na si kwa MUISLAMU au MKRISTO anaweza akafikiria wewe ni mcha mungu KIRAHISI  akikutana nawe KANISANI au MSIKITINI kuliko akikutana na wewe unatoka BAA kujifunza kuacha kunywa pombe ingawa labda huko KANISANI na MSIKITINI uendacho kufanya ni jinsi tu ya kujifunza UTAPELI au kumendea TOTO zuri?


Na labda NI MTU  yuleyule ,...
...HATA NIKIBISHA,....
......na haki ya nani kila MTU umjuaye  anapande  NYINGI mbalimbali,...
..... na wakati kwa MWINGINE ni JAMBAZI,...



...labda kwa wengine wamuonacho na wamjuavyo huyo ni BABA , rafiki au hata SHANGAZI tu  na uhisiyo ya ufisadi WAKE  au tu ujambazi wao ni vitu ambavyo hata hawavifikirii wakati wamfikiriaye ni huyohuyo mtu UMFIKIRIAYE KWA UJAMBAZI au urahisi wa kuvua chupi  mahali pengine ambako hakuna choo.:-(





Swali:

  • Si unajua kuna MAENEO  MCHA MUNGU na mwabudu SHETANI  wanafanana kitu  hata kama  KWA WENGI ni kawaida kujaribu kuamini hao ni watu wawili tofauti?


Ndio,...
.... kuna UPANDE mwingine  wa MTU huyohuyo ambao sio wa jinsi umjuavyo,...
... na jinsi  umjuavyo MTU kunaweza kuwa KUNAATHIRI jinsi ambavyo ungeweza kustukia upande mwingine wa HUYOHUYO mtu.:-(



Swali:
  • AU?
Ndio,...
.... ni vigumu kwa watu fulani wamfikiriaye PAPA JOHN PAUL kama mkuu wa kanisa au hata NYERERE kama RAIS wa nchi ,...
.... kumfikiria katika engo a.k.a  ya  kuwa hao NJEMBAZ kama WANAUME  kuna wakati walichokuwa wanafikiria  labda ilikuwa ni DEMU tu na jinsi BODE lake lilivyokaa  linatia matumaini ukionja labda lazima utanogewa:-(




Nawaza tu hapa MHESHIMIWA na wala usikonde mtu wangu!:-(

Hebu Werrason akatizie denge kwa -Wabelo



Kassav warudie- Syé bwa



Nuru ajaribu kutuliza tena mshawasha kwa kurudisha tena PUNTA MUSIC hapa kijiweni katika-Bounile



Au tu NURU arudie tu -Bunabou

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Unknown 4:16 pm  

Alie tonesha kidonda, ndie huyo huyo anayekitibu...sisemi amejiongezea majukumu!!!

Ngoja nipange namna ya kupita katika barabara iliyo na magari mengi yatoayo moshi mweusi mwingi tangu la na hadi la huko kusikoonekana na na ndio hivyo kunafikika.

Nisubiri.

emu-three 7:27 am  

Mhh usidhani vyote ving'aavyo ni dhahabu, na uzuri wa pilipili nje ndani kuchungu.
Mkuu ni hoja nzuri sana hii, sio wote waitwao watakatifu ni watakatifu au sio, na sio wote waitwao mashehe ni mashehe, na sio wote waendao kanisani au msikitini ni wacha mungu!
Ni hoja muendelezo, shukurani mkuu

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP