Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SHENZI rais NYERERE, shenzi rais MWINYI, shenzi rais MKAPA, na SHENZI RAIS dokta KIKWETE!:-(

>> Friday, January 28, 2011


Lakini ,...
...wakati KUNA WAFIKIRIAO natukana WAHESHIMIWA ,...
.. kwa kuwa nimeandika ,...



   ``......
.....SHENZI Juliasi NYERERE, shenzi alihasani MWINYI, shenzi rahisi MKAPA, na SHENZI dokita KIKWETE!´´       ,....
... labda kwa kuwa wao ni SURA tu ya JAMII ya WATANZANIA,...

...wait a minute,...


.......KWANI hivi ni kweli MAPUNGUFU ya jamii ya TANZANIA ni makosa tu ya VIONGOZI wa TANZANIA?
Ndio,...
....Lakini bado INASEMEKANA ,....
....KULAUMU  au KUTUKANA kwa kawaida NI kutamu kama alaumiwaye NA ANAYETUKANWA  ni mtu mwingine tu !:-(




Ndio,...


... bado ni kweli NAWAZA TU hapa na kwa bahati  MBAYA wakati nafikiria mchango wangu kwa TANZANIA ni nini,...
.......hasa wakati najua MCHANGO WANGU hata kwa NDUGU ZANGU labda ni mdogo sana,....

.....bado najiuliza:


  • Kwani ni vibaya hata wewe ukifikiria LABDA SIO KWELI kila tatizo ni la wengine na wewe labda umechangia HATA KIDOGO angalau   HATA KATIKA kusababisha UMENASA BADO KWA mpenzi wako mwenye  sura MBAYA ila mtamu  au YULE mwenye  sura nzuri ila SIO MTAMU?
Ndio,...
... labda kuna nafasi za watu ZIWAPAZO nguvu zaidi ya kutoa MCHANGO MKUBWA zaidi hata kwa IBILISI,...
.... lakini bado ni kweli kiadoado  hata wasio na nguvu wanaweza kuchangia yasiyokaa mkao wa KIIBILISI!::-(




Swali:
  • AU?
  • Ila MCHANGO MKUBWA na mdogo  unafikiri ni kitu  BINADAMU awezacho kujua wakati tunajua  kuna michango isifiwayo kuwa ni mikubwa ambayo haichukui muda kuna kitu kina bumbuluka kuwa ilikuwa MICHANGO USHUZI MTUPU wakati michango midogo midogo kama ya kumchekea mtu ikaokoa maisha ya mtu kwa kumfanya mtu  afikirie angalau anasababu za kuishi kwa kuwa  angalau bado wajanja wanamchekea au ile ya kumpa tu mtu UBUYU na hata sio KEKI  ambayo ikasababisha muuza UBUYU aendelee kuwa na kazi?



Ndio,...
.... kuna mchango mpaka  WA michango midogo kweli kama michango ya vielea ndani ya shahawa ,...
.... ambayo HAKI YA NANI HATA UKICHUNGUZA kwa kuwa HUNIAMINI utagundua kuwa  huzaa SAA NYINGINE NYINGI bonge la  uwezekano wa BONGE la MIMBA!:-(




Na samahani  WAHESHIMIWA hasa  NYIE akina NYERERE kama mmenuna kwa kuwa nimetanguliza SHENZI mbele ya MAJINA yenu!:-(




Nawaza tu hapa MHESHIMIWA kwa staili ya UjingaBUSARA.....
Na hebu tuhame BASI wazo  MKUU nisije kupandisha mtu jazba bure !:-(


Na hebu EDDY MURPHY atusaidie kulainisha kwa vipengele kutoka kwenye sinema yake ya COMING to AMERICA kwa kuwa nasikia kuna baadhi ya wajanja vichekesho vya nguli MZEE JANGALA havipandi!:-(

... na kwahiyo,...


...basi BWANA hebu EDDY MURPHY aanze na bendi yake iitwayo SEXUAL CHOCOLATE akiwa kama RANDY Watson katika...




Tuendelee na COMING to America na..



Au tuangalie alichokuwa anatabiri EDDY MURPHY kama ni kweli katika..




Au tu tupate The Randy Watson Experience warudishe ustaarabu na kutuliza jazba za BAADHI ya watu watishwao na neno SHENZI kama tu watishikao TU  na  wale  WATAFSIRIO kuna  uwezekano JAMAA sio MHESHIMIWA kisa kacheua neno  KUMAMAYE !,...   kwa kitu - Hang On In There


12 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 12:59 am  

Hivi tukiangalia kwa undani, huwa tunawalaumia nini Viongozi?

Simon Kitururu 1:26 am  

@DA MIJA: Haki ya nani saa nyingine mie sijui kuhusu hilo,...


....ingawa kuna wakati nilikuwa nashabikia sana Rais MWINYI kwa ruksa LABDA alikuwa hajui afanyalo na hakuna waliofaidika! na NYERERE ndio alikua anapatia kila kitu ingawa karibu watu wengi niwajuao najua waliathirika na BIDII zake!:-(

Fadhy Mtanga 7:45 am  

....halafu utakuta mtu hataki kujituma kufanya kazi ili awalaumu viongozi ingawa kiukweli viongozi wengine wanastahili kulaumiwa sana espeshali huyo jamaa huyo!

Simon Kitururu 8:11 am  

@Papaa Fadhy: SI ndio hapooooo!:-(

Albert Kissima 8:14 am  

Huyu raisi huyu, huyu, anastahili lawama! Watanzania kwa kiwango kikubwa wanajibidisha, lakini katika mazingira gani? Nini maana ya uongozi, upo kwa manufaa gani? Uongozi hauna budi kuweka mazingira mazuri ya kumfanya mwenye juhudi stahiki kufaidika na juhudi zake. Kwa tanzania yetu, hili halijawezekana, juhudi muafaka za watu zinakwamishwa na uongozi mbovu, usiojali wananchi.

Ni vigumu sana kwa mimi kuwaza nitalifanyia nini taifa langu kama uongozi ulio madarakani unaoratibu michakato ya taifa langu hautaniwekea mazingira mazuri ya kutumia juhudi zangu ili hatimaye niweze kulitumikia taifa, kujitumikia na kuwatumikia wananchi.

Zaidi, watanzania tunakuzwa katika dhana ya "struggle for existance" na "survival of the fittest", namshukuru Mungu kumekucha, nikipata ugali chumvi, siku inapita, ilimradi watu wamekata tamaa, maana juhudi zao zinakwamishwa kila uchao.

Simon Kitururu 8:21 am  

@Mkuu ALBERT:SI ndio Hapooooo!:-(

Mija Shija Sayi 10:57 am  

Hivi mnasemaje juu ya ile staili ya Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani? Labda ndiyo inafaa nchi yetu au?

EDNA 1:29 pm  

Mkuu umenena nilishangaa kuona vijana na manguvu yao wanapoteza muda wao wa thamani kwa kushinda vijiweni.Na wababa nao asubuhi asubuhi wanachaza Bao...

Lakini pia kuna vijana ambao wanajituma sana mfano siku hizi kuna hata wanaume wanachoma vitumbua kazi ambayo miaka ya nyuma kazi kama hiyo ilionekana kama ni ya wanawake.

emu-three 1:36 pm  

Duuh, nilishituka kidogo, nikatizama nyuma kuwa hakuna `gwanda la polisi...' maana ....mmmh, hiyo lugha uliyoanza nayo mkuu, ungekuwa huku bongo, sasa havi, ungelisikia
'Riweke ndani hiroo, rinamtuka rimkuu ra nchi...'
Mkuu kweli sijiu nisemeje...hali ngumu, maisha mgumu, lakini mwisho wa siku naona sie wenyewe tumejitakia..sasa cha moto tunakiona...!

Christian Bwaya 1:45 pm  

Du kweli hii treni ya mawazo. Hivi uliwaza nini kuwaza hivi?

Hatufanyi wajibu wetu, tunatafuta wa kumlaumu! ndio!
Hilo (la kulamumiana) linaanzia katika ofisi zote ndogo ndogo mpaka ile Kubwa ya karibu na feri.
Kila mtu anamlaumu mwenzie mpaka tumefika mahala hata Bwana Mkubwa anatulalamikia wanakaya.

Sasa swali: kama kila mmoja anakwepa kuwajibika, nani anahusika?

Kumbe pamoja na kwamba kila mtu ana nafasi ya kutimiza wajibu wake, matokeo ya "hiyo mitimizo ya wajibu" inatofautiana kutokana na ukubwa wa "influence circle". Yaani kuna miborongo ya wengine hutanua tatizo na kulifanya lisambae mithili ya kipundupindu kutoka raia mmoja mpaka mwingine.

Wapo ambao "ushenzi wao" una athari kubwa kwa wanajamii wengine kuliko "viushenzi" vidogodogo vya raia wa kawaida!

Kwa hiyo, utabaini "shenzi Mkodo" si sawa na "shenzi Mkwere"

Yasinta Ngonyani 1:52 pm  

Nilipoanza kusoma nilistuka nikasema moyoni Mtakatifu vipi leo? lakini baadae nikaona ni sawa tu. Tatizo watanzania hatutaki kujituma kwani tukijituma na viongozi labda wangeona mfano huo nao labda wangefanya kazi kama inavyotakiwa.

Simon Kitururu 8:41 pm  

@Da MIJA: Labda!:-(

@EDNA: Si ndio hapooo!:-(

@Mkuu BWAYA: Pamoja na yote ,...


tukiingilia mpaka kinena ``Kwa hiyo, utabaini "shenzi Mkodo" si sawa na "shenzi Mkwere"!:-(


DUH!:-(

@DADA YASINTA; Hivi kumbe huwa unanisoma!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP