Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Poleni wote mliokumbwa na mikasa ya kisiasa ARUSHA!

>> Friday, January 07, 2011

Nawasiwasi na hatua siasa ya Tanzania ilipofikia!:-(



Watu wanazidi kuchoka Tanzania nzima!
Watu hawana MATUMAINI !

 Na wasio na tumaini hata na SERIKALI YAO ,....
.....tusishangae wakichukua hatua mkononi kudai haki zao.:-(
Ni wakati wa VIONGOZI wetu kuwa makini sana,....
....kama nia ni kurudisha amani Tanzania kwa kuwa kuna uwezekano sifa ya AMANI Tanzania sasa hivi imebaki kuwa ni stori tu kama zile za zilipendwa!

Na hekima na BUSARA vitawale ,...
... na sio ubinafsi na mambo ya utajiri wa harakaharaka!



Mungu ibariki Tanzania!


Na NI HILO TU!:-(

Hebu JCB and Arusha All Stars warudie kinu-Arusha

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:56 am  

Sio wewe tu Mt. hata mie nina wasiwasi au sijui ndo mwisho wa dunia? Mungu ibariki kweli Tanzania yetu....

EDNA 12:45 pm  

Mwaka umeanza vibaya,ni kweli watu wamechoka na hawana imani tena na nchi yao,machafuko huwa yanaanza hivi hivi,tunaomba wale wenye mamlaka wafanye kazi yao kurudisha Amani.

Unknown 1:16 pm  

Na mheshimiwa JK akumbuke kuwa alikabidhiwa nchi ikiwa ni ya AMANI. Watu wamechoka! Na sasa damu yamwagika. Na si ya kuku...

Simon Kitururu 1:33 pm  

@WOTE: Yani basi tu!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP