Wakati nahisi YA WENGINE ni manono zaidi na NAHISI ukiyabonyezabonyeza ni KITU freshi SANA yani !:-(
>> Tuesday, January 04, 2011
Wakati na WIVU na NATAMANI kuwa kama watu WENGINE,.....
.....ya WENGINE huvutia,....
...... yao yana VYEO, ushujaa na hata NGUO NZURI kuliko mie.:-(
Wakati natamani kuwa kama watu WENGINE,...
....ya WENGINE vitu hupatia,.....
...... yao huonekana YANA MAFANIKIO ZAIDI, nyumba nzuri na hata furaha kuliko mie.:-(Swali la kujitia moyo:
- Hivi si labda ni kweli mwenye wivu ni kipofu kwa alionealo wivu?
Wakati natamani ya WENGINE,.....
.... ni ya WENGINE yale yenye kunivutia,......
.... ambayo nabobea katika kuyachungulia hukutayari AKILINI nimeshajijengea kuwa YAO hayana kasoro kwa kuwa WENGINE siwachunguzi kasoro katika yao kama nijichunguzavyo mie.:-(Swali tena:
- Hivi si kwa ya wengine ni RAHISI kustukia tuyafikiriayo ni MABAYA kuliko YETU au tu yale tudhaniayo ni MAZURI kuliko YETU na kusahau ni jinsi gani hayo yako tu kama YETU?
- Na hivi si inasemekana kunauwezekano ni rahisi zaidi KUONA ya wengine kuliko yako?
Lakini,.....
.....LABDA,......
..... kwa wengine ,.....
...... yako ni MENGINE,.....
..... na KWAO kwa kuwa hawakujui wanaweza kuwa NAO wanatamani YAKO au tu wawe kama WEWE,.......hasa kwa kuwa yako yanaonesha kama vile ni BOMBA ZAIDI au angalau tu limpenzi lako ZURI ZAIDI utafikiri halinyi vile.:-(
NAWAZA TU Mheshimiwa!:-(
Hebu tudeku STOMP
Au tu Oliver N'GOMA aingilie tu shughuli kwa - Sal'
Au tu Oliver N'goma aendelee tu pia na-Julie
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
nanukuu "Na hivi si inasemekana kunauwezekano ni rahisi zaidi KUONA ya wengine kuliko yako?"mwisho wa kunukuu:- hii nimeipenda kwanikweli kabisa
Wakati unatamani ya wenzako na wapo wanatamani ya kwako, wakijua wewe yako ni bora kuliko ya kwao. Kuna usemi unasema, ukitaka maendeleo tizama aliye juu na ukitaka ubinadamu tizama aliye chini!
@Da Yasinta: Tatizo ni kwamba KWELI ni kitu kigumu kwa kuwa UKWELI saa nyingine ni vile tu vifananavyo na tufikiriavyo ni KWELI.:-(
@M3:Tatizo ni ,....
.... hivi ni nani aliye JUU au CHINI kama tukizingatia utashi wa BINADAMU katika kuamua ni nini kiko katikati ,...
....wakati twajua mpaka kuna aaminiye hapohapo India kuwa MUNGU ni Ng'ombe , mwingine ni ALLAH , BUDHA, Sir GOD au tu ..... kwa mtizamo wa KIBINADAMU wa binadamu aaminiye mzani wake wa kupima mambo uko sahihi?
Mmmmhhh au kaaazi kwelikweli!!!
kweli unawaza. I love this post.
Post a Comment