Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WAKATI kuna WATU wamekaa KIMYA huku wanafikiri WANASHUHUDIA mtu ANACHEMKA!:-(

>> Tuesday, January 11, 2011

NDIO,...
.... labda kuna WATU bado WANAONGELESHA MTU  mpaka kuwa,......
..... suruali yake IMENING'INIA  chini sana ya tako na chupi iliyoingia mnato ile chafu  inaonekana,....
........ kwa kukaa hivyohivyo KIMYA!:-(


Swali:

  • Unafikiri kwa kukaa KIMYA wafikiriao Simon Kitururu ANACHEMKA hawaongei kitu akistukiacho  Simon Kitururu?




Ndio,....
...amini USIAMINI,....
.... lakini KUKAA KIMYA labda ni staili tu MOJA WAPO ya kuongea,.....
...... na kama MTU yuko makini anaweza kustukia anaambiwa kitu na kuelewa vizuri tu  maoni ya  ALIYEKAA KIMYA,.....
.... na HAPA simaanishi  kustukia yale marahisi  tu  ya ALIYE KAA KIMYA yastukiwayo kirahisi  kama yale yaliyozoeleka KUSTUKIWA kuwa aliyekaa kimya  kwa kukodolea tu MACHO KIFAA MURUA  anaweza kuwa anasema KIFAA MURUA lakini  kina bonge la MATEGE , mwanya kama mfereji wa maji machafu au tu mtu  ANA BONGE la makalio a.k.a SANGARA WAMO  kama kifurushi cha mihogo kwa staili ya  kiutepwetepwe,.....
.... kwa kuwa ALIYEKAA KIMYA ukisikiliza vizuri  na kama MAKINI  pia unaweza kustukia MTU anaweza kuwa anasema,....
..... ama kweli MWANANGU umepotea ,...
...na yote hayo ANAWEZA KUWA ANASEMA kwa kukaa KIMYA TU  vilevile tu.:-(



NIWAZO TU HILI MHESHIMIWA!:-(


Hebu ZAP MAMA waingilie kati wazo kwa -Iko-Iko(Suca Mama)





Au tu ZAP MAMA warudie pia -Sweet Melodie


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP