Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUGUNA wakati TAMU na wakati kuna AGUNAYE wakati CHUNGU au tu wakati ANABISHA!:-(

>> Saturday, January 22, 2011

Kuguna ni KAULI,....
..... na kama unabisha GUNA,...
...... uone kama hakuna atakayeelewa au angalau KUFIKIRIA  kwa kuguna kwako,.....
..... labda  unasikilizia UTAMU!:-(

KUGUNA ,...
..... ni ushahidi hata ule usio NGUNA,...

.... na labda kuna  MTU kwaweza kuokoa mpaka MAISHA YAKE kwa kuhakikishia watu kuwa ingawa hajambi huyo MTU bado yuko HAI na hata kama  hajambi  anapumua  na katika kuishi wakati huo hasikii UTAMU.:-(




Swali:
  • AU?


KUGUNAAAA!:-(




Ndio,...
....ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(






Hebu Banana Zorro aingilie shughuli tu kwa - Zoba





Au tu Tshala Mwana asawazishe tena kwa -Dezo Dezo




6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 9:17 pm  

Kitururu ungezama kwa undani kidogo kutofautisha namna hizo 2 za kuguna. Mimi sijaelewa bado somo vizuri.

Mija Shija Sayi 1:53 pm  

Kitururu je unamaanasha ile kauli ya Matondo ya chakula kitamu na kichungu vyote vinaweza mfanya mlaji kukunja uso?

emu-three 12:09 pm  

Mguno, ni kuonyesha kukubali, kushangaa, au kukataa...
Nimekuambia uende dukani, sasa unaguan nini...'
Ndio kuna kuguna kwa namna nyingi, lakini yote ni mguno, uwe wa raha au karaha, uwe wa utamu au uchungu!

chib 1:20 pm  

Mguno mara nyingi kama sio zote ni ishara ya kukataa, kushangaa au kupingana.
Mguno wa kukubali du! Labda kwa wapare kama sijakosea?

Rachel Siwa 7:38 pm  

kaka Kitururu mara nyingi unakomenti kwa kuguna sasa wewe ukiguna unamaanisha nini? kukataa,kunogewa,kushutushwa au kukubali?.

Simon Kitururu 8:07 pm  

@Mkuu Malkiory: Tatizo la luingia undani mambo mawili kwa kawaida huzaliwa mambo matatu mapya kwa undani huohuo. Na sijui kwanini nimeridhika kwa taralila yangu ilioamsha ndani yako kwa kuwa nahisi kuna kitu umewaza na kwangu hiyo ni KUELEWA.:-(

@Da MIJA: Unamaanisha ile iliyofanya MKUU Mwalimu MATONDO kubadili jina la BLOGU YAKE?

Hapana simaanishi vile lingekuwa bonge la JIBU LANGU,...
... kama ningejua kwa uhakika Frof.Matondo alikuwa anamaanisha nini kwa UHAKIKA!:-(


@M3:

Haki ya nani sina lakukubishia katika hili!:-(


@Mkuu CHIB:

Naamini miguno yako yote ingerekodiwa LABDA ungejishangaa:-(

@Rachel wa SWAHILI na WASWAHILI:

Mara kibao huwa namaanisha sina lakusema na ku-TAG hiyo post ili watakao comment wengine wasemacho kije kwenye simu yangu ki-email hata kama bado sijarudi kwenye hiyo BLOG.:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP