Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

``KAWAIDA´´ -labda ni AINA ya kilevi ukizingatia MTU hakawii kung'ang'ania kufanya afikiriavyo kwake ni KAWAIDA hata kama ni SUMU !:-(

>> Friday, January 14, 2011

Yasiyo kawaida kwa mtu ,....
... ndiyo awezayo kuyaita MATUSI:-(

Ya kawaida kwa mtu,...
... ndiyo yale wengine huweza kuona ni UVIVU wake au tu pia MATUSI:-(

Na kwa kuwa  CHA KAWAIDA ni kile alicho kizoea mtu,...
..... kwake atakirudiarudia na kama ni CHAKULA cha KAWAIDA   atajaribu kukikwepa tu siku za sikukuu ambako atajaribu kubadili MLO  hata kama sio matusi.:-(



Swali:
  • AU?



Kitu kikigeuka KAWAIDA  kwa mtu,...
... yaweza kuwa ndio chanzo  cha MASIKINI kuendelea kuwa MASIKINI.

Mapenzi yakigeuka KAWAIDA kwa mtu,...
... labda ndio mwanzo wa MKE au MME kutonogewa sana na mlo wa sikukuu kugeuka kuwa ni yule KIMADA au tu MTU wa nje wafanyayenaye kazi OFISI MOJA hata asiyejua kaingilia mahusiano ya WALIOWAHI KUWA wapendanao ambao bado wanaishi pamoja masikini!:-(

Swali:
  • SI unajua kawaida kwako labda kwangu  nadhani ufanyacho ni MATUSI kama ilivyo kawaida  kuandika kwangu kirahisi iwezavyo kuwa kwako ni MATUSI?
  • SI unajua LABDA  chochote huweza kugeuzwa KAWAIDA?


KAWAIDA!:-(




Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


Ijumaa na WIKIENDI NJEMA MHESHIMIWA!


Hebu AL GREEN abadili kwa -Love and Happiness




Hebu AL GREEN abadili tena kwa -People get Ready




Au tu hebu ZIGGY MARLEY arudie ndude hiihii- People get ready

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 1:45 pm  

Kawaida ni ndugu yake mazoea, hawa walikuwa kama mapacha, lakini ikifika muda kawaida akaona abadili tabia, akachepuka pembeni, ..
Ndio mkuu, mambo yaliyozoeleka huwa yanakuwa `ni kawaida tu' hata kama hayana `utamu' na kama yana utamu ule utamu husiha na kuleta `kichefuchefu' lakini ni `yule yule kawaida. Wengine ndio hawo wanamkimbia Mazoea na kutafuta nyumba ndogo.
Ni hayo tu mkuu

chib 7:58 pm  

emu-three, naona umedadavua kwa ustadi :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP