Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Sijui ndio ukubwa huu?:-(

>> Wednesday, January 05, 2011

Yani  hivi karibuni,....
....watu wengi wanatutoka a.k.a WANAFARIKI ambao nawajua!

Mpaka kuna wakati hivi karibuni nikaanza kukwazika kuweka kipengele cha R.I.P hapa BLOGUNI kwa kuanza kufikiri mwisho BLOGU hii itageuka ya maombolezo ki R:I.P kila siku!:-(

Yani nikichukulia tokea Dr REMMY Ongala atutoke tu mpaka leo kwa upande wa wanamuziki ni kibao niwajuao wameanza,...

... na hapa siongelei  wale kama akina Dr Billy Taylor, TEENA Marie ,..... na BOBBY wa BONEY M watokao nchi za mbali,.....
....ila ni mpaka tu Mustapha Ngosha

Tukitoka huko,....
..... nikajaribu kufikiria majirani zangu pale MOROGORO,....
..... yani  karibu kila nyumba kuna mtu nimfahamuye  kashaanza!:-(

Na nikikumbuka kuwa utotoni ,....
....jinsi MAREHEMU walivyokuwa wanahesabika ,....
.....mpaka leo hii ambayo nikiulizwa namba ya MAREHEMU niwafahamuo hata kwa kuruka watu kama akina Rais NYERERE ambao ni maarufu ntashindwa hesabu,....

......najiuliza sijui huu ndio UKUBWA au nini tena.:-(

Nachojaribu kusema:

Kama siye ni waaminio MUNGU :
....labda TUKUMBUKE tu kushukuru angalau kwa UHAI  TU tulionao kwa maana hatujui ni kwanini SISI TUPO na wengine wameshaanza!

NI HILO TU MDAU!

Hebu JHIKOMAN aturudishe Bagamoyo kwa-Set me free

Au tu Jhikoman aongelee-Kuagana

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

malkiory 4:00 pm  

Kituturu, usijeogopa kama jamaa mmoja ambaye alipatwa kulazwa hospitali moja hivi, jina nimelisahau, kilichotokea ni kwamba kwa bahati mbaya jirani zake walikuwa wakiaga dunia moja baada ya mwingine hadi kubakia yeye pekee yake, alichokifanya jamaa ili kuokoa maisha yake ni kutimua mbio kwani alijua zamu inayofuata ilikuwa ni yake! Hahahaa.

Yasinta Ngonyani 4:06 pm  

Mt. unaogopa?

Simon Kitururu 4:17 pm  

@Mkuu Malkiory: :-)

@Yasinta: Siogopi!Nitafakari tu a.k.a reflexion tu za maisha mtu wangu!

John Mwaipopo 5:44 pm  

mkuu usiogope ni kawaida. unavyokuwa unapanua horizon ya kuwajua watu wa sehemu nyingi kijijini, wilayani, mkoani, nchini na duniani. pengine kamjamaa mlikozaliwa tarehe moja pale kijijini kajunjumele hakajapata kujua vifo vingi kiasi hicho. anakumbuka vifo viwili ama vitatu tu katika kipindi hichohicho.

ila wanamuziki wamepukutika baada ya remmy kufariki.

Rachel Siwa 5:52 pm  

kaka nakandamiza katika maneno ya mwisho Tumshuru Mungu!! Amina kaka Kitururu!.

Anonymous 7:15 am  

Yah, maisha ndivyo yalivyo, jema nikumshukuru mungu kwa hali aliotupa, kwani waliotangulia mbele za haki sio kuwa walijua, sio kuwa wanamakosa, sio kuwa wanapendwa zaidi na muumba, bali kila mtu ana siku zake za kuishi hapa duniani, hiyo ndiyo imani ya dini.
Kufa kweli kila anaogopa, hiyo sio siri, lakini kufa ni lazima, jambo jema ni kuomba `mwisho mwema' na tukumbuke kuwaombea waliotangulia, kwani `vitabu vyao vya matendo hapa duniani vimefungwa' ...
Ni hayo tu mkuu. Na kikumbuka sana hicho kisa mkuu Malkiory...!

emuthree 7:16 am  

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP