Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UPYA-wakati kuna wadaio MTUMBA ni MALI MPYA kama tu MPENZI wa MTU MWINGINE ambaye hajawahi kuwa wako alivyo kwako BIKIRA!:-(

>> Friday, January 14, 2011

UPYA mara nyingi hukosewa ,....
.... kwa kulinganishwa na UBORA,....

..... wakati kuna VIFAA kibao kama unataka kuviona makali yake kipembejeo,...
... basi weye labda usikimbilie shughuli huku ukiwa na  KIFAA kipya.:-(



Swali:
  • Unabisha?
Ndio maana ukitaka kushindana KUSKETI kwenye barafu huwa huiingii kwenye barafu na VIATU vipya,...
.... na hata kama ni kulima kwa jembe la mkono,....
.... jembe likimbiliwalo mara nyingi sio lile jipya kabisa,...
... kama tu katika SINDIMBA kiongozi wa kunengua mara karibu zote huwa sio yule ambaye katika unenguaji mbele za watu ni mpya!:-(

Swali:
  • Unabisha?


Kuna hatua MTU azipitiazo katika kuizoea hata CHUPI ya mtumba mpya ,....
.... iliaache kufikiria ilikopitia na roho kutulia kuwa kweli sasa ni chupi yake na wala hainukii kimtumbamtumba na kwake ni chupi tu MPYA!:-(

Na kwa kawaida ni siku KADHAA tu hutosha kusahaulisha mtu kuwa gwaguro la MTUMBA mpya ,...
.....kimtazamo fulani LABDA halikuwa  kitu KIPYA





Swali:
  • AU?

Korodani za hoja niilengayo:

Labda ukweli ni kwamba umuhimu wa UPYA wa kitu chochote kile,....
.... hujengwa KISAIKOLOJIA TU zaidi,...
... na ni ni UBONGO TU  unatafsiri umuhimu wa UPYA na ni nini KIPYA,....
.... ndio hasa kilichopo nyuma ya ashangiliaye UBIKIRA wa MTU katika kutafsiri huo kama aina ya upya,KWA ashangiliaye NYUMBA MPYA , simu au tu vitu vingine ,...
.... hata kama ukweli uko palepale kuwa labda kitu bora wala sio kile KIPYA.

Swali:
  • Si unajua kuna VIDHANIWAVYO VIPYA na kuna VITU VIPYA ambavyo vinamchezo wa kuchukuliwa viko sawa?



Kwa hiyo:
UPYA wa KITU kutokana na kuoanishwa USAFI wa kitu, KUTOKUWA na hatia,.....
......labda sio busara kuuoanisha na UBORA wa kitu.:-(


Na tukitoka kwenye UPYA WA KITU  na kuingia kwenye UPYA WA FIKIRA za MTU,....
....faida KUBWA ya kuanza kufikiria UPYA ni kwamba kuna kitu tayari unajua ni mkweche hasa baada ya kustukia fikira za mwanzo hata kama ni zile za UJAMAA na KUJITEGEMEA hazikufanya kazi.:-(

Ingawa chakusikitisha ni kwamba kwa mtu,...
...... labda hata katika kuanza kufikiria UPYA ,...
....kunauwezekano wazo halitakuwa jipya sana kwa kuwa kunauwezekano mkubwa wazo JIPYA bado litakuwa limeathiriwa na lile WAZO la zamani kitu kiwezacho kufanya wazo lidhaniwalo ni JIPYA kuwa na kasoro kama tu zile za WAZO  la zamani.:-(

Ila tu ,...
...FAIDA ya kuanza UPYA mara nyingi ni kubwa kuliko kung'ang'ania kilichoshindikana cha zamani,...
.... kwa kuwa bado MUANZA UPYA angalau kuna kitu anajua alichokosea mara ya kwanza au hata ile mara ya tisa.

Swali:
  • Uko tayari kuanza UPYA?
  • Na si unajua labda ni kweli MPENZI asiye wako kwako ni MALI MPYA na nibikira hiyo kwako?


UPYA!

Labda mwisho wa yote UPYA ni michezo na tafsiri ya UBONGO,...
..... na chakula chako cha zamani utupacho jalalani KWA KUFIKIRIA UZAMANI WAKE  labda kwangu ni bonge la  mbolea MPYA kwa ajili ya chakula changu kipya.:-(

Ni wazo tu HILI Mheshimiwa!:-(

Hebu ATM vifananishwe na CHOO katika kubadili hali ya hewa hapa KIJIWENI



Les Little ft MANU DIBANGO wadinye- Ressens le son




MC Solaar arudie -Caroline



Au ngojea tu tena Buju Banton na Wayne Wonder warudishe tu- Bonafide Love

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 1:50 pm  

Mhhh, eti mkuu ulisemaje vile??? Oooh, ndio mtumba kwetu ni mali mpya hasa ikiwa ndani ya fashion, siunajua tena kwetu kuiga. Hata jinsi iliyochakaa huku kwa vile alionekana `ten cents' au twenty nanihii kaivaa, basi ni fashion,
Siunakumbuka yule mpiga mziki aliyechelewa kuingia jukwaani, akiwa na kwa nanihii, akaurupuka na kuvaa suruali ya nani wake, ikawa inampwaya.
Basi alipofika jukwaani kila akiserebuka suruali hiyooo...basi wabongo wakaona ni fashion. Ipo siku mmoja ataingia jukwaani na chupi kichwani wabongo tutaiga...ndio fashion....
Nimewaza tu mkuu, sijui nimetoka nje ya mada!

Simon Kitururu 10:33 am  

@M3: Hukutoka kwenye mada Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP