Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

WATU wafikiriavyo MTU alivyo VS ukweli kuhusu ALIVYO mtu!

>> Thursday, January 13, 2011

Yasemekana,....
....DAIMA kuna tofauti  kati ya afikiriwavyo MTU,....

..... na ukweli wenyewe wa jinsi alivyo kweli MTU.:-(


Na ni hatari kama kirahisi TU bila uhakika MTU,....
.....kwa jinsi tu AMFIKIRIAVYO mtu,.....
.... akafikia KUAMINI ndivyo kweli ALIVYO mtu.:-(


Swali:
  • Si labda ni BORA mtu kukumbuka kuwa yale baadhi yajulikanayo ya MTU labda bado sio UTHIBITISHO WA KWELI ni wa aina gani  huyo MTU kitu kiwezacho kufanya baadhi ya wafikiriwao wataenda MBINGUNI labda kuna watakao pata bahati ya kukutana JEHANAMU?

Ndio,....
....labda yale baadhi tuyajuayo kuhusu MTU,....
.... ndio chanzo kipotoshacho na kuingiza udhaifu wa MTU kumjua MTU,...
... kwa kufikiria  kuwa  kidogo tukijuacho ndicho kitoacho mwangaza halisi na picha yote nzima kuhusu alivyo MTU.:-(


NIWAZO  TU hili MHESHIMIWA!:-(


Hebu The Temptations waendeleze kwa KITU  fanki  -SHAKEY GROUND

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 1:41 pm  

Mtu alivyo kwa sura, inaweza ikawa tofauti na uhisivyo ndivyo alivyo...mmh, utamuona kijana mtanashati, kavalia safi, tabasamu kwa saana, lakini undani wake mungu mwenyewe ndiye ajuaye, hata chupi yake ina afadhali...mmmh nii hayo tu mkuu!

Yasinta Ngonyani 2:42 pm  

Na wengine wakafikiri msichana ana sura nzuri, macho kama golori na tabasamu nzuri kumbe tabia yake ovyo au kinyume chake...kwa hiyo tusiwafikirie watu kama wanavyoonekana tuwafikirie kama walivyo. Akheee naacha ...

Rachel Siwa 5:59 pm  

Nilipokuwa mdogo nikipishana na mtu mwanaume mnene na mweusi mwenye macho mekundu na makubwa nitatoka nduki nikifika nyumbani nasema jamani nimekutana na jambazi!!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP