Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati ile kitu ``KILA KITU NA MAHALI PAKE´´ inavyoweza kugeuza kukaa uchi pekee chumbani au chooni kwa MHESHIMIWA ni kitendo cha HESHIMA kwa kuwa inadhaniwa TU huko ni MAHALA pake!:-(

>> Saturday, January 15, 2011

Ndio,....
.... kila kitu na MAHALI PAKE ,...
.... imewezesha BAADHI ya  wakaao UCHI hadharani  kudhalilika,...
.... kisa kuna waaaminio TU wakaao  uchi  HADHARANI wanakosea eti kwa kuwa yasemekana hapo hadharani kuonyesha dalili za MAKENDE au tu MTUNO WA SEHEMU ZA KIKE   sipo MAHALI PAKE.:-(

Swali:

  • AU?


Lakini  wazo a.k.a AIDIA  ya kila kitu na mahali pake,...
.... labda sio sahihi ,...
.....kwa KILA KITU,...
...ukizingatia labda   mahali sahihi pa kitu ni pale kitu kinapofiti NA LABDA ni WAKATI UKO CHOONI au tu kwenye DALADALA ndipo uhitajipo zaidi KUSALI kuliko idhaniwapo SALA ni MAHALI PAKE kule KANISANI , kwenye sinagogi , CHINI YA MBUYU  au tu mpaka kule MSIKITINI.:-(


Kila kitu na mahali pake,...
....kumbuka USAHIHI WAKE kwa kawaida  hutokana na  MAWAZO YA MWANADAMU TU  hasa  kutokana na alivyoathirika katika KUJIFUNZA KITU ,...
.....na kajifunzaje NINI na WAPI ni SAHIHI ,...
....... na labda kwa kuzingatia hilo  LA BINADAMU NA MAFUNZO YAKE  unawezagundua na KUELEWA ni kwanini BAADHI ya mila zilichelewa mpaka kuamishia CHOO NDANI YA NYUMBA kiselfukonteina  kwa kudhania  NI  SAHIHI ZAIDI  mahali paitwapo MSALANI lazima pawe nje YA NYUMBA kwa kuwa  AIDIA ya KULALA HUMOHUMO na kunyea HUMOHUMO ni moja ya kitu  KUTOKANA NA KILIVYOCHUKULIWA KUKOSA USAHIHI  kiliweza tosha kufanya watu  kujiuliza ashauriye kujenga choo ndani ya nyumba HIVI AKILI YAKE ina hali GANI.:-(






Swali:
  • Si unaweza kustukia  ni kwanini kuna waliozinguka na busara na USAHIHI wa  watu kunyea mumohumo  kunyumba walalako hata kama ni chumba kingine?
  • Sasa unadhani ni kweli kila kitu kwa  HEKIMA UZIJUAZO ZA KIBINADAMU walipomulia watu kuwa ni MAHALI PAKE hapawezi kugeuzwa KIBINADAMU na kuwa SIO MAHALI PAKE ukizingatia karibu  katika vingi kama sio kila kitu -``KILA KITU NA MAHALI PAKE´´  ni  tungo tu na ubunifu wa akili dhaifu za KIBINADAMU?

Ndio sibishi,...
.....labda kila kitu na mahali pake,...
.... na kistaarabu kuna ambayo hufanyika  kirahisi JIKONI kuliko kule  kufanyiwako WATU wafanyayo kuwa ni siri  ingawa kila mtu anayajua,...
... kule MSALANI.:-(

 Ndio,...
.... bado labda ni staili tu ya kukaa uchi HADHARANI ifanyayo baadhi ya watu kudhania kukaa uchi HADHARANi sio mahala pake,...
... wakati staili tu ya kukaa uchi ikibadilika unawezakuta kuna WAHESHIMIWA wengi tu watakaoridhika  kuona uchi kistaarabu  HADHARANI.:-(



SAMAHANI naendelea kuwaza......!:-(
Na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(


Hebu Ella Andall aingilie kati kidude kwa - Rhythm of A People



Au tu Sister Phumi akatizie denge shughuli kwa - Africa




Manu Dibango atokezee kwenye kona naye na -AFRICA



Au tu twende Angola tukagawiwe kidude pana -MARIKA

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP