Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kawaida KIMOJA huanzisha KINGINE na HATUA kwa HATUA mwisho wa siku kuna MBUZI anaweza kujikuta na MIMBA!:-(

>> Saturday, January 22, 2011

Ndio,...
.... MAMBO mengi  hayatokei GHAFLA,...
...... na  ni hatua kwa hatua  ndizo  zilizomtoa PROFESA MBELE  shule ya MSINGI na mpaka kumfikisha kwenye UPROFESA,...
...... kama tu  adokoaye MBOGA hatua kwa hatua ziwezavyo  kumfikisha  kuhitimu hadi UJAMBAZI.:-(


Swali:
  • SI unajua  KUFANYA kidogokidogo ndio mwendo wa KUIZOEA hata DHAMBI?


Na ni kwa hatua kwa hatua,....
... ajifunzaye ULEVI atafanikiwa kuwa MLEVI,....
.... MALAYA   atajulia ni akijisikiaje na mahali gani umalaya huwa mtamu,....
..... aliaye ofisini KIFISADI atajulia staili ya kuonekana MHESHIMIWA ingawa mwizi,....
..... au  tu ilivyo kuwa ni kwa  HATUA  kwa hatua  tu siku moja  mtu anavyoweza kufikia KUELEWA mtu asiye MUELEWA kama vile SImon KITURURU!:-(




Swali:

  • AU?
Ndio,...
.... labda si GHAFLA tu Rais KIKWETE  akafikia kuwa RAIS,...
... kama tu  ilivyokuwa sio ghafla  tu ukajifunza nini ni MATUSI!:-(







NAWAZA TU HAPA MHESHIMIWA!:-(
Jumamosi NJEMA MKUU!


Hebu Richard Dawkins adadavue kitu-On Morality




Prof. Richard DAWKINS aendelee kwa ndude- Absolute Morality





COCOA TEA akatizie denge mbadilisho wa wazo na kulainisha  kwa shughuli -Come again





Au tu Gregory Isaacs arudie - Cool Down The Pace

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 1:58 pm  

Na hii ni safi sana hasa kwangu mimi binafsi, umenikumbusha na kunitia nguvu maana nilishaanza kuanguka...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP