Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Adolf Hitler; Ukweli Uliofichika…..(1)

>> Saturday, October 01, 2011



Na Nova Kambota (Mwanaharakati),


Nimekuwa nikifanya utafiti kuhusu maisha ya Adolf Hitler kupitia
maandiko mbalimbali  na niseme wazi katika dunia ya leo  “mwendawazimu
mkubwa”  ni mtu anayepingana na fikra za kimagharibi ndiyo kwa wasomi
wetu wa sasa wenye mtazamo wa kizungu ni vigumu kuyaona mambo katika
uhalisia wake bali katika mtazamo wa kiulayaulaya na Marekani.
Maandiko na mtiririko wa mantiki unabainisha kuwa fikra za anayeitwa
dikteta Adolf Hitler zingalipo mpaka leo hii tena zinaongoza sio tu
Ujerumani bali Ulaya na Marekani, pengine kuna watu watapinga hili ,
ila sina hofu, najua kwanini watanipinga? “hawasomi” na “hawapendi
kusoma” na zaidi wamefumbwa wasione vinavyoonekana, naam! Naandika
kuibua mjadala, naandika kunyoosha palipopinda, naandika ili tujifunze
kufikiri.


Kama unadhani fikra za Adolf Hitler zimekufa au wazungu hawapendi
mawazo yake nasema basi hesabu “Maumivu” narudia tena hesabu maumivu,
kabla hujaendelea kubisha hebu tafuta kitabu cha Adolf Hitler
kinachokwenda kwa jina la “Mein Krampf” kilichopigwa chapa mnamo mwaka
1925. Mwenyewe Adolf Hitler alikiandika kitabu hiko akiwa gerezani
mnamo mwaka 1923, inaelezwa kuwa kitabu hiko ndiyo ulikuwa mwongozo wa
utawala wake baadae kuanzia mwaka 1933 mpaka 1945.


Baada ya vita kuu ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945 pengine kwa
kukusudia au kwa hulka yao ya kuficha ukweli wazungu na wamarekani
wamefanikiwa kuficha ukweli kwa zaidi ya miongo mitano kuwa “fikra za
Adolf Hitler ndiyo mwongozo wa mataifa hayo ya kibeberu” na vyovyote
itakavyokuwa ukweli utabaki hivyo kuwa Mein Krampf(My Struggle) au kwa
Kiswahili kinaitwa “Mapambano Yangu” ndiyo mwongozo wa Ulaya na
Marekani kwa maana nyingine tunaweza kunyumbulisha mantiki kwa
kuhitimisha kuwa “Mawazo ya Hitler yanaitesa Afrika mpaka leo”.


Ukipitia kitabu hiko utakutana na kauli hii “Those who want to live,
let them fight, and those who do not want to fight in this world of
eternal struggle do not deserve to live.Adolf Hitler
Mein Kampf”  kwa tafsiri nyepesi ya Kiswahili Adolf Hitler hapa
anamaanisha wanaohitaji kuishi hawana budi kupambana, na wale
wasiotaka kupambana basi hawastahili kuishi Dunia hapa.  Naam! Haya
ndiyo mawazo ya kiongozi wa Manazi Adolf Hitler , sasa je hebu tuone
undani wa kauli hii na je nani anaitekeleza kwa vitendo? Na kwa mapana
yapi?


Mpaka leo hii hakuna ubishi Ulaya na Marekani wako katika mapambano ya
kufa na kupona kuhakikisha ubeberu wao unazidi kuimarika na zaidi ya
yote mirija yao ya kunyonyea inazidi kufyonza maliasili za Afrika .
Mapambano ya wazungu ni kuhakikisha kuwa Afrika inaendelea kuwa
masikini, haya ndiyo mawazo ya Adolf Hitler ambayo yanakumbatiwa na
mabeberu wa Ulaya na Marekani, wasiyapende vipi wakati yanawasaidia?
Sasa kwanini wadanganye dunia kuwa hawampendi Hitler? Waswahili
wanasema “ukipenda boga sharti upende na ua lake”, Je iwapo ni kweli
Hitler ni mbaya kwanini wakumbatie na kuzisujudu fikra zake?  Kuna
nini hapa?

Naam! Hii ndiyo kwanza sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii ya
kusisimua , jiandae kusoma sehemu ya pili itakayoeleza kwa undani
uhusiano kati ya mawazo ya Adolf Hitler na ubabe wa mataifa ya Ulaya
na Marekani. Asante kwa kusoma!




Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa
Saturday, October1, 2011.

Nimetumiwa na:
...Nova Kambota

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 2:34 am  

Kambota! Kambota! Kambota!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP