Hongera WANAWAKE wa shoka ELLEN JOHNSON SIRLEAF, Leymah Gbowee na TAWAKKUL KARMAN kwa kutunukiwa tuzo la NOBEL!
>> Friday, October 07, 2011
Ellen Johnson Sirleaf RAIS wa LIBERIA |
Mwanaharakati wa Ki-Liberia Gbowee |
Mwanaharakati, Mwanasiasa na Mwanahabari waki-YEMEN Tawakkul Karman |
HONGERA ZENU akina MAMA!
Habari zaidi kongoli HAPA
Ngojea nilolome kidogo!
Tukiachana na kuwa hili TUZO la NOBEL kama tu kwenye sinema lilivyo la OSCAR mie huzinguka nalo kwa kuwa huwa naamini kuna ajenda za chinichini ZIKIWEMO zile za KISIASA na KIMIKAKATI ZAIDI ambazo hufanya maamuzi ya nani ashinde na kwa hilo kufanya kuna mpaka akina Rais OBAMA kutunukiwa NOBEL kitu ambacho siamini kama walistahili,....
.... bado labda lina mchango wake kiaina ukizingatia BINADAMU akihusika katika chochote kile labda bado kitakuwa na mapungufu ya KIBINADAMU!
MWISHO wa MLOLOMO!:-(
Hebu tubadili mshawasho kwa kumuachia Dama Ludmila aturudishe tena Luanda ,ANGOLA na kuanzisha upya kwa - Acaba de Dar o Toque
Dj Sottão aingilie kati na -Sentido Silencio
Dj Sottão aendeleze mwanzo wa wikiendi hii kidhambidhambi tena kwa-Moço direito
Au tu dhambi ikae njenje tu katika siku hizi ambazo labda nizamwishomwisho,...:-(
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
HONGERA ZENU AKINA MAMA...SIKU MOJA LABDA ITAKUWA ZAMU YAKO KAKA sIMON AU LABDA YANGU ...ila sijui nifanye nini mpaka nipate hiyo..LOL
@Yasinta:Cha muhimu bado ni kuwa TUZO zuri la kutenda wema amablo ni zuri kuliko yote wala halihitaji mtu mwingine akutunukie!
Kama ni mtendaji wema tayari TUZO unalo MOYONI hata kwa ufikiriayo ni MADOGO kiwema!
Matunzo mengine ya kupewa na BINADAMU WENZAKO yana udhaifu wa KIBINADAMU hata kama tuzo lenyewe ni KUPEWA Utakatifu na PAPA wa KANISA!
Simon! ni kweli unajua wengi nikiwa mmojawapo tunasahau ulilolisema: Ahsante kwa kunikumbusha.Ungekuwa karibu...basi naacha.
Wanawake wana weza basi tu kulialia kwao ndo tatizo ila wakinyamaza mambo yanakuwa.hongereni sana wanawake,ambao ni mama zetu,dada zetu, wakezetu,wachumba,nk. Lakini sasa hao kwenye kideo hiyo bwana kitururu dah! ! manake huo muziki mpaka unaacha kunoga unabakia kuwa chabo hao ma dada na vinasa upanti/vichupi mweeee sijuwi ni kijiji gani katika moja ya nchizetu katika bara la afrika.nimependa sana uchezaji wao kwenye maji,wameumbika hakika ni warembo.kaka S.
@Yasinta: Tuko Pamoja!
@Kaka S: Mdau moja kutoka LUANDA , ANgola aliniambia hapo ni umbali kama kilometa 30 kutoka Luanda mjini ndiko walikorekodia kideo hiki.
Simon na kaka Samam:-(
Post a Comment