Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati TONY MELENDEZ asiye na MIKONO anapiga GITAA kwa MIGUU!

>> Friday, October 07, 2011

Swali:

  • Si kuna wafikiriao unahitaji mikono kupiga GITAA?

Hebu baada ya kusikia kifupi kuhusu yeye  ashushe pini:
-Let it be


Tudeku tu  pia  na yaliyojiri    PAPA John Paul akiwepo kushuhudia  katika kibao,....
- Never Be The Same


Ndio,...
.... labda kuna GITAA  lako KIMAISHA  ambalo limezoeleka kupigwa mimba  hata  KIPESA au tu KIVYETI  vya ELIMU KUBWA ,...
.....lipigikalo bila PESA wala ELIMU  kama utatumia kitu kingine  kulipa mimba tu LIZAE NEEMA kwa kutumia visivyozoeleka!

Swali:
  • AU?

Ndio,...
.... labda UNAWEZA udhaniacho huwezi,...
..... ila JARIBU kwa njia nyingine  kama NJIA watumiazo wengine kwako HUNA jinsi ya KUWANAZO!

Ni hilo tu MKUU!
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA!

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 1:06 pm  

mfano huu wa huyu jamaa ni shule tosha,kwa sisi binaadamu ambao hujiita tumekamilika!!?. hakuna kisicho wezekana hapa duniani kama unania ya kweli.ukiwezeswa inawezekana.muhimu nikujuwa hasa nini unataka,na kwa uhakika niwewe ndiyo muanzishaji ,na siyo mwingine mara nyingi matatizo yetu husemelewa na watu wengine bila kuwa na uhakika kama ndivyo hivyo sisi wasemewa tuna taka.huwezi kukaa ofisini na kusema (kiongozi)mlemavu/walemavu lazima wapewe vibasikeli,je umeenda kuonana nao na waka sema baisikeli ndiyo wana taka? ya wezekana mmoja wao ana hitaji magongo. tushuke tuwafuate waliko tusemenao tutagundua mengi. nimeipenda hii video. Kaka S.

Simon Kitururu 2:01 pm  

@KakaS: Nakunukuu kipengele ``....mara nyingi matatizo yetu husemelewa na watu wengine bila kuwa na uhakika kama ndivyo hivyo sisi wasemewa tuna taka.´´ -mwisho wanukuu.

Yani hapo umegonga kabisa penyewe Mkuu!

malkiory matiya 2:23 pm  

Mwingine anayeniacha hoi ni Jimi Hendrix & teeth solo.

Simon Kitururu 2:37 pm  

@Mkuu Malkiory:Jimi Hendrix kiboko aisee!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP