Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati Rais KIKWETE leo anatimiza Miaka 61

>> Friday, October 07, 2011

Swali la kizushi:

  • Hivi ni WATANZANIA wangapi hawajui tarehe ya siku waliyozaliwa?



Rais Kikwete alizaliwa tarehe SABA mwezi wa KUMI mwaka 1950  ,...
.....kijijini Msoga, BAGAMOYO , TANGANYIKA.

Happy Birthday Mr Rais!

NI HILO TU!






Au tu tena Mighty SHADOW aingilie kati na kubadili mchezo mzima  kwa-You looking for horn




Mighty Sparrow akatizie denge kwa - Water de Garden



Au tu Mighty ARROW ajaribu kuzima kwa-Hot Hot Hot



Kabla  tu Lord Kitchener  hajazima tena kwa - Sugar Bum Bum



10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

sam mbogo 4:26 pm  

Mtakatifu,usipime wengi tu siku za kuzaliwa nitatizo. hata haya mambo ya kusherehekea siku ya kuzaliwa,nisikuhizi, nawapongeza akina dada wao ndo huwa mstari wa mbele katika hili.pia wao ndiyo hutukumbusha .lakini najuwa kwanini imetuchukua muda sana kuwa na utaratibu wa kusherehekea siku ya kuzaliwa.wengi wetu hatupendi kujulikana umri wetu hivyo ukifanya sherehe watu watakuuliza na itakuwa sooo.tumpe hongera raisi wetu,kwa kutimiza miaka61 si mchezo na hapo nikiongozi!!? kaka S.

Simon Kitururu 4:37 pm  

@Kaka S: hapo nyuma niliwahi kuandika kuhusu swala hili zima la kupongeza watu katika tarehe zao za siku waliyozaliwa na kugusia kuna watu hizi tarehe ziongezekapo wala sio kitu cha kufurahia.

Na mie binafsi sio msherehekeaji wa siku yangu kitu ambacho kilishawahi kutatiza wadada kadhaa maishani mwangu kwa kudhani sithamini juhudi zao zakuniandalia suprise party na vidubwana vilaliavyo muelekeo huo.

Na nikweli ni WADADA wakumbukao sana ndude hizi ila chaajabu hasa huku ughaibuni ni Wadada waongozao kwa kutotaka kujulikana miaka hasa wakisha gusa miaka ya thelathini hivi. Na ukimuuliza mdada hapo miaka yake inakuwa kama vile umemuuliza uzito katika jamii hizi ambazo kilo kibao kiunene ni siri kuwa LIDADA sio zuri -kitu kigeuzacho swali kugeuka tusi:-(

Ila HONGERA zake Mr Pdezidenti wetu aisee kisababu kama ulizotonya Mkuu!

emuthree 4:43 pm  

Mkuu tupo pamoja ndugu yangu, ingawaje ndio hivyo, ...sijajua kuwa mambo yatakuwje...

Yasinta Ngonyani 4:48 pm  

Hongera Rais Kikwete kwa kutimiza miaka 61....Ila nina swali kwako Mtakatifu kwanini wewe ulipotimiza miaka hukubandika hapa kwako? unaweza kuacha kujibu ...ni udadisi tu wa kapulya!!!

Simon Kitururu 4:56 pm  

@Yasinta: Soma jibu langu kwa Kaka S paragraph ya PILI mstari wa kwanza kuna jibu la ulichouliza.

Pili sioni sababu ya kusherehekea kwa kuwasikuomba kuzaliwa na nahisi sinauwezo kiutawala ufanyao nimefika siku hata ya leo hii. Kitu kifanyacho sioni umuhimu wa kusherehekea wala kupongezwa kwa kitu ambacho labda hakiko chini ya uwezo wangu -ambacho waaminio MUNGu hudai ni cha mapenzi ya MUNGU tu niko hai.


Kwa hiyo naamin Mimi kama Simon Kitururu sifai kupewa Hongera kwa kufikisha siku ya kuzaliwa wakati labda sijahusika kihivyo ili kuwezesha kuwa hai siku hio. Na pili sina uhakika kama ni sahihi kumpa Hongera Mungu kwa kufanya awezacho kirahisi kama MUNGU cha kuamua niwe HAI au nife kama wafao sasa hivi wakati naandika kukujibu.:-(

umedaka MADAILEMA yangu katika SWALA?

Yasinta Ngonyani 4:59 pm  

Nimekupata:-(

sam mbogo 7:05 pm  

Hivi mmeshashitukia, miaka unayo pewa/kuandikiwa katika kumiliki pasipoti ni kipimo tosha cha maisha yako hapa duniani.maana mimi huwa pass yangu ikiisha huesabu ni muda gani umepita na kukuta ni uhai tosha wa mtu,na nichukuapo nyingine kwa miaka tena ijayo hujipa tumaini la kuishi tena kwa kipindi hicho cha umiliki wa pasipoti hiyo ya kitanzania.sijuwi nyinyi wengine mnaoaje ? nikama zaidi ya besidai unayo sherehekea kila mwaka. au nimewaza vibaya. kaka s

Simon Kitururu 7:42 pm  

@Kaka S: Unajua sikuwa kupima muda kihivyo Mkuu! DUH usemalo kweli kabisa!

Yasinta Ngonyani 9:30 pm  

Kaka mkubwa na mdogo hata mimi sikufikiria hilo kwa kweli...ila nina kastory kamoja siku moja nilimuuliza baba mmoja una miaka mingapi akanijibu ngoja nikaangalia kwenye biblia yangu....na pia nikamuuliza una watoto wangapi akajibu vivyo hivyo...ujanja eehhee!! au ?

Goodman Manyanya Phiri 10:34 pm  

Hongera Raisi Kikwete!

61, Kama ni miaka, ni mingi sana na umebarikiwa kuliko hata huyo ndugu yetu tajiri Steve Jobs (who died at 57).


LAKINI.....!


20=Kama ni miaka ulilala mfulilizo bila kuamka mithili kobe, Mzee Kikwete=20 miaka aisee!

(“Kama huu sio uvivu basi sijui uvivu ni nini!”)



44562=Kama ni milo miwili kwa siku: sitahesabu bakuli za ugali naweza nikapigwa marufuku bure Tanzania=44562 milo ya mtu mmoja tu!

(“Sasa watoto wengine waTanzania wale nini?”)



Hata hivyo, Mheshimiwa Raisi, sinamshangao hata kidogo kwanini wewe ni kiongozi wa nchi yako kwani nawe unayo mengi ya kwako MAZURI uliezaliwa nayo kwa siku hiyo ya Jumamosi tarehe 7 October 1950 kama ifuatavyo:


"Saturday's child ('ruled' by Saturn) – Wise, professional, subdued, dedicated, practical and/or morose, suspicious, complaining, jealous, timid”

http://www.elbertwade.com/page84.html)

HAPPY BIRTHDAY, YOUR EXCELLENCY!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP