Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

``Halafu nikajisikia vibaya kwa kuonja TAMU ila ni ile HARAMU´´-hata KISTORI!

>> Saturday, August 27, 2011

Kuna wajisikiao VIBAYA kwa kuwa tu WAMEJISIKIA vizuri,...
..... kwa kufanya au KUONJA waliyojifunza kuwa ni MABAYA.

Swali:
  • SI unajua ASIYEPENDA hata UGALI WA MUHOGO anaweza kufunza mtu mwingine kuamini UGALI wa MUHOGO ni MBAYA?

NDIO,...
..... labda yawezekana ni MUHIMU kukumbuka labda mengi yawafanyao WAPENDAO kujisikia vibaya baada ya KUONJA hata kama hapa hatuongelei wale waonjao KIDUDE haramu kisa hakijabarikiwa bado na SHEKHE ,mchungaji au ASKOFU ,....
.... yasemekana MABAYA na imani ya nini KIBAYA mara nyingi ni MASWALA tu ya KUJIFUNZA hasa kama hayo mabaya ni yale yasiyo sumu kikuua MTU.:-(

Swali:
  • Unafikiriri ni vitu vingapi kwako ni VIBAYA kisa tu UMEFUNZWA kuamini ni VIBAYA bila kushuhudia UBAYA wake?
  • Na sinasikia pia BANIANI ni MBAYA ila kiatu chake ni DAWA kitu ambacho kinaweza kutetewa na kufikia kumfanya mtu afikirie labda BANIANI sio mbaya hivyo kama kiatu chake kwako ni ASPIRINI?


Ndio,...
.... kuna waonjao hapa DUNIANI na kufurahia LADHA ya WAONJACHO,....
..... ingawa hujisikia vibaya baadaye hasa kwa kuwa wamependa walichoonja ,...
... ila bdo hata kama LADHA ya hicho KINANILII ni TAMU ,...
.... bado ni HARAMU.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
JUMAMOSI NJEMA!







Hebu Hawa Pullo abadili kwa - Pulaku



Salif Keita na Cesaria Evora wasibadili sana mwelekeo aliotupeleka HAWA kwa-Yomore





Baaba Maal arudishe ndude- Niiwa




Kabla Salif Keita hajamalizia kwa ndude - Africa



2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 4:39 pm  

Duh! kaazi kwelikweliii!! Jumamosi njema nawe pia Mt. Simon:-(

Simon Kitururu 5:49 pm  

@Da Yasinta: Asante Mtu Wangu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP