Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Unavyokifikiria UNACHOKIFIKIRIA sasa hivi hata kama ni MKE wa JIRANI,....

>> Monday, August 29, 2011

.... labda  hutakifikiria hivyo tena MAISHANI,...
.... hata kama KIJINA unachokifikiria ukikifikiria tena kesho ni HICHOHICHO,...
.... mwendo wake kama bata!:-(

Swali:
  • AU?
  • Si unajua labda wakati unafikiria huwa unasahau kustukia jinsi unavyofikiria?


Ndio,....
.... labda kama hujastukia  kustukia ufanyacho ni KUFIKIRIA,....
...... wengi hawastuki kuwa wanafikiria  na kwa hilo hata waufikiriavyo MLENDA MWAKA juzi hawatastukia ni tofauti na waufikiriavyo MLENDA  leo!

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Hebu tu Miguel arudie ghafla  - Quicke



Musiq SoulCHILD arudie - Halfcrazy



Musiq Soulchild aongezee dozi kwa-BUDDY





Dwele aingilie kati kwa kudai tena-I'm Cheatin´



Au tu tena Slum Village wamalizie kwa - Tainted


4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 10:42 am  

Dondoo la leo limenifanya niwaze mkuu, hivi kweli kama kila kitu mtu anachokifikiria kingekuwa kinaonekana kwa kila mtu ingekuwaje, mbona watu `tungeaibika' labda kungelikuwa na jinsi ya kusitiri hizo fikira kama tunavyovaa nguo...NI WAZO TU MKUU!

Anonymous 1:17 pm  

Kufikiri,ni muhimu,bila fira huta injoi ulimwengu huu unao kuzunguka. je isha wahi kuwa kweli, kile ulicho kifikria kikatokea/kukutokea.?Kakak S

Yasinta Ngonyani 5:10 pm  

Kufiri ...kuna mtu mmoja aliniambia ni vema kuandika mara tu unapofikiri ukiacha hutakumbuka tena ...hakika naamini kwani kuna siku nilikuwa nimefikiri kitu na nikasema nitaandika au kumbuka nitakapoamka nilipoamka sikukumbuka kabisa...Nachotaka kusema ni kwamba nakupongeza sana Mt. Simon kwa jinsi mtindo wako wa kufikiri:-)

Simon Kitururu 8:35 am  

@M3: DUH yani kama kitu anachofikiria mtu kingekuwa kinaonekana ingelikuwa kazi na fasheni nafikiri ingekuwa ni kuacha macho tu yaonekane ila mwili mzima fulu kufunikwa!

@Kaka S:

Mie maranyingi nifikiriacho HUTOKEA na mara nyingi kwa mfano nikijikuta niko mahali halafu sina sababu maalumu kitatokea kitu ambacho sikutegemea kama vile kukutana na rafiki yangu wa zamani ambaye hata sikujua alipokuwepo na vitu kama hivyo ambavyo hunifanya niamini ndio sababu.

Ila ndoto zangu maranyingi sio kweli! Ila Dada yangu Mkubwa huwa namuogopa kwa kuwa akiota mtu fulani kafa haitachukua muda mtapata taarifa kafa kweli!:-(

@Kapulya:Mie nafikiri hilo la kusahau ni MTU na MTU ! Kuna ambao hawasahau wakiwaza kitu kama tu kunaambao hawasahau ukiwakosea hata baada ya miaka thelasini watalipiza tu kisasi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP