Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa utamu wa UBWABWA unatofauti wakati unaanza kula na wakati umeshiba !

>> Friday, August 26, 2011

Na kwa kuwa yasemekana hata ladha ya Coca Cola  ni tofauti  wakati unaonja mara ya KWANZA,...

.... na baadaye wakati unamalizia chupa ya tano,...
....... si unakumbuka kuwa labda hata ya  MPENZI ,....
.... kumbuka tamu ya mwanzoni  labda haitafanana na ya baadaye wakati MPENZI kageuka mazoea?

Ndio,...
......KITU kilekile kinamsikiliziwa tofauti tofauti aisee ,...
........ na mara nyingine chungu huweza kugeuka TAMU ,...
.... ingawa TAMU na CHUNGU vyote huweza kugeuka mazoea tu!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!





Au hebu Sam Cooke aaanzishe upya kwa- You Send Me





Otis Redding aongelee - Pain in my heart




Au tu Otis Redding amalizie kwa - That's how strong my love is



6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:48 am  

Mazoea hujenga tabia!!

Simon Kitururu 12:03 pm  

Kweli kabisa Yasinta!:-(

Anonymous 1:15 pm  

utamu wakitu ni ulimi wako! Kaka S

Anonymous 2:05 pm  

Swali moja huwa mbona kuna chakula au kinywaji ambacho mtu hukipendelea akiwa na chaguo hilo kati ya zingine? Mazoea kweli hujenga tabia.

Asante kwa mziki, umeongeza utamu wako ingawa...!

kibogoji 5:25 am  

Ya Leo Kali.

Simon Kitururu 5:53 pm  

@Kaka S: Kweli kabisa na ndio maana si wote tupendao CHIPSI MAYAI!:-(

@Serina : Mazoea we acha tu! Na nimekuzoea unajua!:-(

@@Mkuu Shaaban wa Kibogoji: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP