Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunafananisha BUSARA za Rais NYERERE na BUSARA za Rais KENYATTA!

>> Friday, August 05, 2011

Kitu kifanyacho kitu kiwe ni cha BUSARA,...

...... mara nyingi ni swala la MAAMUZI  tu ya MTU  katika  kuhukumu  ni nini ni UJUNGA!:-(

Na misingi ya MAAMUZI  HAYO ya MTU hutokana na ajuayo MTU,...
..... kitu  kiwezachofanya BUSARA kwa WATU wawili TOFAUTI kuwa ni vitu VIWILI TOFAUTI.:_(

Swali:
  • Si cha BUSARA kwa MTU mmoja kwa mwingine chaweza kuwa ni DHAMBI , wizi na UJINGA?

Ndio,...
..... labda BUSARA kwa Rais NYERERE ,....
...... ilikuwa ni UJINGA kwa Rais KENYATTA kitu kilichofanya mmoja wao afe TAJIRI  na bepari na mwingine masikini na MJAMAA wakati nchi yake inakimbilia kwenye UBEPARI.:-(


Swali:
  • Kwani  unafikiri BUSARA kwa FISADI katika kufanikisha UFISADI haiwezi kuwa ni ujinga kwa BAADHI ya wenye BUSARA fulani hata kama hao hatuwaiti  kuwa ni WALOKOLE  waaminio utajiri wa duniani ni wa KIJINGA kwa kuwa mambo yote ni mpwito MBINGUNI  au WAJAMAA waaminio watu wote tujaziwe maharage sawa kwenye kibakuli sawa?

Ndio,...
.... labda BUSARA kwako inategemea umeegemea nini,....
....... kitu kifanyacho labda usijiamini sana kuwa wengine ni WAJINGA!:-(


NI wazo tu hili MKUU na usikonde!

Hebu Proffesor Jay akumbushie - Kama Ipo





 Mood wasogeze pembeni kidogo kwa - Karma




Au Queen Latifah ahamishe tena kwa - Elements I'm Among



Halafu  tu Onyx wamalizie kwa ku-Slam Harder

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP