Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

PENZI yasemekana ndilo lifanyalo wengi waone umuhimu wa kuwa HAI,...

>> Thursday, August 25, 2011

... na pia ndilo lifanyalo watu wapate cha maana cha KUKIFIA.


Na yasemekana ,...
...PENZI  la NDUGU, rafiki, malaya au tu hata la kitu tu fulani,....
....hilohilo NDILO lina misingi iliyowazi zaidi ya CHUKI za MTU ,...
.... kwa hiyo  ukipekuwa CHUKI ZAKO  unaweza kujikuta umevumbua ni nini hasa UNAKIPENDA.


Swali:
  • SI nasikia ukichukiacho labda kinauhusiano wa karibu sana na ukipendacho?
  • Kwani unafikiri  PENZI la BINADAMU limekilo sensi- ni lile lielekezwalo kwa MUNGU wake tu?

Ndio,....
...... labda chunguza zaidi  kwanini unampenda MUNGU!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!

Na hebu Aidonia abadili kwa-Jack Hammer



Au tu Ben Sollee abadili kabisaa mchezo kwa -How to See The Sun Rise

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:04 am  

Nanukuu "PENZI yasemekana ndilo lifanyalo wengi waone umuhimu wa kuwa HAI,..." mwisho wa kunukuu. Swali:- kwa hiyo bila PENZI hakuna uhai kweli?

serina 2:47 pm  

Ahem, maneno yameniishia! :)

Anonymous 4:23 pm  

KUPENDA.Hili neno ni zito sana,sasa sijuwi penzi nini,na kupenda nini.Halafu uhai na mungu,vyote hivi ukiviweka pamoja,na kuanza kuchambua moja baada ya nyingine,unaweza ukajikuta,una jiwekea kautaratibu,ju ya kupenda,awe ni demu wako.mkeo mumeo,bila kusahau mola wako. kwa harakaharaka ndani ya penzi uhai upo,ila pale tu utakapo shilikisha mwili,akili,roho yako. kaka s

Goodman Manyanya Phiri 1:41 am  

@Yasinta


Naam, Bibi! Bila penzi/upendo hamna uhai.


Kiasi cha upendo au penzi (wala sio kiasi cha ujanja-INTELLIGENCE) ndicho kinachotofautisha binadamu kwa viumbe vingine. Wala sio uzushi mtupu wakiBiblia kwamba "...Mungu ni upendo"(1John 4:8).


Kama huna upendo wala penzi UMEKUFA KIROHO na inamaana wewe katili sana na ni mtu mzuri sana kwetu wenye upendo kwani unatupatia fursa safi sana ya kuonyesha upendo wetu tunapowaokowa wale unaowafanyia unyama wako!

emu-three 8:06 am  

Ukijua kupenda na ujue na kuchukia...lakini swali kwanini uchukie?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP