Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wengi wenye uwezo wa KUSIKIA VIZURI ndio waongozao kwa KUTOSIKILIZA MTU hata wakitongozwa!:-(

>> Saturday, August 27, 2011

WENYE uwezo wa  KITU,...
.... yasemekana HUJIAMINI  ZAIDI kitu kifanyacho,.....

..... mara nyingi  wanaingia UDHAIFU wa kutotumia kipaji walicho nacho vizuri kama wale ambao  wana UWEZO MDOGO na ili wawe MAHIRI na KITU inabidi wafanyie kazi  sana kumasta hicho KITU!

Swali:
  • SI umewahi kusikia KIPOFU kama STEVE WONDER akiongelea hata kwenye nyimbo zake yale asiyoyaona kama vile ya uzuri wa MSICHANA MZURI awezavyo kuwa mahiri wa hata wa kusimulia UZURI  wakati unajua hajawahi KUONA?




Ndio,....
.... na kwa kuwa pia UNAONA VIZURI,...
..... labda hicho ni moja ya KITU kikigezo kifanyacho HUANGALIII VIZURI VITU,...
.... kitu kiwezeshacho kuna uwezekano utafutacho hata LEO umekipita kwa kuwa HUANGALII VIZURI kwa kuwa tu unaamini UNAONA VIZURI.:-(

Swali:

  • Kwani huamini kuwa ni kweli WASIOONA VIZURI ndio hasaaa wenye jitihada zaidi ya KUANGALIA VIZURI hata uzuri wa PKIPENGELE ambacho kinaweza kuwa sio PAJA?

NDIO,...
.... tukiacha mengine,....
......labda ni KUJIAMINI  kwa WAONAO na WASIKIAO VIZURI,....
... ndiko ambako kunachangia WAONAO kutoangalia na WASIKIAO kutosikiliza WANAAMBIWA NINI.:-(

Swali:
  • Si unajua KUSIKIA na KUSIKILIZA ni vitu viwili TOFAUTI?
  • Na si unajua KUONA na KUANGALIA ni vitu viwili TOFAUTI?

Ndio,...
....ni wazo  TU HILI MKUU!


Hebu Gregory Isaacs aingilie kwa -Dance This Reggae Music



Gregory Isaacs akumbushie ya - Slave Master




Gregory aingizie ya -Night Nurse



Gregory Isaacs asiondoke bila kuachia - My Only Lover




AU tu hebu MAKASSY abadili mchezo mzima kwa kuturudisha Tanzania kwa ndude -MAMBO BADO



Ndio bado,...
... nakatiza hapahapa Amsterdam!:-(







































0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP