Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukikaa sana na walio UCHI hata kama wewe umevaa kificha nyeti/ NGUO,....

>> Saturday, August 27, 2011


... yasemekana utaanza kuonekana kama hao WALIO UCHI ,....
......utaanza KUFIKIRIA kama haohao unaokaanao ambao wako UCHI,...
.......na mwisho utaanza KUJISIKIA  kama walio uchi kabla ya wewe mwenyewe kuanza nawe kukaa UCHI!:-(

Swali:
  • Si unajua hata ukikaa sana na walio MALAYA unaweza kujikuta umeuzoea UMALAYA na labda kuanza kufanya UMALAYA wewe mwenyewe bila kustukia ufanyacho ni UMALAYA?
  • Na si inajulikana kama unataka MOTO wako wa KILOKOLE uendelee kuwa kilokole labda ni busara kujichanganya zaidi na WALOKOLE kwa kuwa unaweza kuyeyusha hata USWAHILINA kama wewe ni MSWALIHINA ila ni yule ashindaye na wasioamini ya KISWAHILINA?


Ndio,...
...... labda kama unataka sana KUELIMIKA,...
..... labda jichanganye SANA na WALIOELIMIKA,...
.........na kama unataka usijizoeshe DHAMBI au tu kukaa uchi kwepa kujichanganya sana na waliodhoea kufanya dhambi au tu kukaa uchi,...
.... kwa kuwa hata yale UYAONAYO NI ya AJABU huzoeleka ukijichanganya sana na walioyazoea.

Swali:
  • Si yasemekana hata KUUA kunazoeleka na aliyewahi kuua MARAMOJA kurudia kuua mtu sio shughuli kubwa sana kama ilivyokuwa mwanzo?


Ndio,...
.... ukikaa sana hata JALALANI,...
..........nasikia jalala litaanza kuzoeleka pia AISEE!:-(


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!





Hebu  Israel Vibration waingilie kati kwa kudai-System not working




Burning Spear arudie-AFRICAN POSTMAN



Burning Spear aongezee dozi kwa-African Teacher




Au tu Culture wabadili tu kwa - Peace, Love & Harmony



Ndio nipo AMSTERDAM ,Uholanzi ..
.... na kwa bahati mbaya nakatizia denge maeneo pia :-(







































0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP