Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MABONDIA KUZIPIGA SEPTEMBA 4 MWANANYAMALA

>> Sunday, August 14, 2011

MABONDIA wa ngumi za kulipwa Ramadhan Shauri na Bakari Dunda wataoneshana kazi katika pambano lisili la ubingwa litakalofanyika Septemba 4 mwaka huu.

Pambano hilo ambalo litakuwa la raundi nane litasindikizwa na burudani kutoka katika kundi la 'Makhirikhiri wa bongo' huku likitanguliwa na mapambano manne ya utangulizi ambapo yatafanyika katika ukumbi wa CCM Mwinjuma wa Mwananyamala Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe 'Bigright' alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na kuwataka wadau wa mchezo wa ngumi kuweza kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia mapambano hayo.

Bigright aliyataja ambambano ya utangulizi ni kati ya Anthon Mathias na Shabani Madilu ambapo pambano lao litakuwa la raundi sita.

Wengine ni Joseph Mbowe na Ezekiel Ezekiel raundi nne, Isa Omari na Kade Hamis raundi sita na Sadat Miyeyusho na Herman Richard raundi sita.

Pia wamo Yona Miyeyusho na Haruna Said raundi nne, Martine Richard na Jumanne Kilumbelumbe raundi nne na pambano la mwisho litakuwa kati ya Mwaite Juma na Franck Pury raundi nne.


Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao.

DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi

-- Habari hii ni kutoka kwa :

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP