Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ikibidi, HAKUNA chaguo na achaguaye hata cha kuchambia labda HAJALAZIMIKA huyo!

>> Sunday, August 21, 2011

NA ikibidi na unaumwa njaa hakuna HARAMU ,...
.....na hutachagua hata CHAKULA weye.:-(
Swali:
  • Si  unajua UKILAZIMIKA ustaarabu  huwekwa pembeni hata na sistaduu na sio tu yule MSTAARABU yakhe?
  • Si labda uchaguzi ni LAKSHARI na walazimikao  hawangojei hata kupigia mtu KURA ili wachukue chao?

Ndio,....
...... labda chaguo hata la nini ni cha KUCHAMBIA kama tu ni wapi PAKULALA ,....
...... ni la ambaye hajalazimika kuchamba kwa kuwa ukilazimika chochote na sio tu ukuta wa choo cha stendi ni KICHAMBIO na sehemu yoyote inafaa kulala kama UMECHOKA KISAWASAWA na unahitaji KULALA hata kama chakulalia  ni JIWE na eneo ni msalani!:-(

Swali:
  • Si kuna uwezekano WATANZANIA  bado wanachagua kwakuwa bado wanalakshari za kuchagua kwakuwa HAWAJALAZIMIKA bado na WANGELAZIMIKA  wasingerembesha kwa kulalamikia tu machaguzi kwa kuwa wangeshachukuwa vyao MAPEMA?
Ndio,...
.... inasemekana IKILAZIMU,...
.... ustaarabu huwa unawekwa PEMBENI!:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
JUMAPILI NJEMA!

Hebu JEAN-PHILIPPE MARTHELY  aanzishe tena tamutamu  kikubadili wazo kwa -Bèl kréati






Patrick SAINT-ELOI adai- Eskizé mwen



JOCELYNE BEROARD arudie- Kay manman



Jacob Desvarieux aje na Vick na Bayce katika-BOTCHO



Jacob Desvarieux aendeleze kukuna kipele kwa- Mwen Enviw




Jacob Desvarieux aongezee dozi kwa - Gorée



Kabla JEAN CLAUDE NAIMRO hajaingilia kati kwa ndude iliyotuna - AVÈ'W DOUDOU



Au tu huyuhuyu  Jean Claude NAIMRO atulize tu na kufunga mjadala  kwa-A Toute


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP