Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kuna WAFIKIRIAO wanapenda UKE haimaanishi kila apendaye UKE hana mwalimu wa jinsi ya kupenda UKE au tu EMBE DODO!

>> Tuesday, August 16, 2011

Ndio,...
.... labda kuna AFUNDISHAYE MTU jinsi ya KUFIKIRIA mpaka jinsi ya KUPENDA ,....
... na katika kufikiria unapenda MCHICHA kuliko NYAMA ZA KUCHOMA,....
..... pamoja na yale yote yajulikanayo kama ya MTOTO kuzaliwa tu na kujua TITI la MAMA ni TAMU kimapenzi ya MAZIWA yatokayo kwenye  bonge la nyonyo la mdada,...
.... bado yawezekana ukikua utastukia kama TITI la MAMA ni tamu labda UTAMU wa UJI ni jambo la kujifunza na ukizoea UJI baada ya kufunzwa utamu wa UJI ili uache maziwa ya MAMA,...
.... labda maziwa ya MAMA si MATAMU kihivyo kama huta jifunza upya KUYAPENDA!:-(


Swali:
  • Kubwa zima ,-umeshaonja maziwa ya MTU ukubwani na ukafikiria ni matamu kama MAZIWA?
  • SI unajua hata ukiwa na uhakika na jinsi unavyofikiria  na KUJIAMINI ufikiriavyo ni SAHIHI kivyakovyako -labda umejifunza kutoka kwa wengine kuwa afadhali ufikirie kivyako na uhitimishe mambo kivyako kwa kuwa jinsi ulivyojifunza kufikiria wengine WANACHEMSHA?



Ndio,...
... katika KUFIKIRIA,...
......kila MTU anaweza KUFIKIRIA,.....
.....lakini jinsi ya kufikiria MAMBO,...
..... labda hata ya jinsi gani WALI ni mtamu labda kila MTU ana MWALIMU kikujengea ladha fikira hizo kiutamu wake uchiuchi!:-(

Swali:
  • AU?


Na ufikiriavyo hata TITI, tako au tu GARI  gani JIRANI yako analo katika kukutishia maisha kisa mpenzi wako anapenda MAGARI,....
....inawezekana ni MATOKEO ya shule ndefu tu ya KUFIKIRIA iathirio mpaka LADHA iliyoanza ulipozaliwa tu,....

.......na WALIMU hata usiowatambua kiualimuwao katika kufikiria KWAKO  hata labda UGALI WA MUHOGO ni mtamu kuliko PILAU ya MSIBANI,....
.....kama TU wale wajambao sebuleni na kujibaraguza kama sio wao kitu ambacho kinafanya na wewe mpaka siku hizi unaachia ushuzi mpaka mikutanoni kikazi na kujibaraguza sio wewe,...
..... kwa kuwa UMEJIFUNZA VYEMA ,...
.... labda mpaka jinsi gani UNAFIKIRIA NI KILO NGAPI ZA UJINGA nimeziandika kwenye TARALILA hiii,...
.... una MWALIMU!:-(

Swali:
  • Unafikiria ni kweli MMOJA wa WALIMU WAKO ni WEWE?
  • Na unafikiri kila malaya silaha za umalaya  WAKE hata wa KIUME malaya alikuwa na MWALIMU? 

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Jumanne njema MHESHIMIWA!


Hebu tupitie tena TOGO ili Bella Bellow aanzishe kwa -O Senya



Seal aanzishe tena upya kwa-Crazy



Halafu huyuhuyu SEAL amalizie kwa -This Could Be Heaven


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP