Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MSONDO NGOMA yatwaa tuzo la The Best Rhumba Group katika EAST AFRICA MUSIC AWARDS

>> Sunday, August 21, 2011

super d.jpg
Super D
BENDI ya muziki ya MSONDO NGOMA  imepata TUZO la The Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards -katika mkusanyiko wa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya MSONDO
kuibuka kidedea katika mashindano hayo-mashindano yaliyofanyika Nairobi, Kenya -athibitisha  meneja
wa bendi Saidi Kibiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D.

Na msemaji wa bendi SUPER D alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanalionyesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhihirisha kuwa bendi ipo ngangari popote duniani maana bendi imekamilika kila idara .

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na
sikukuu ya Iddi inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D aliendelea kusema kuwa  bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja
vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hilo la Afrika
Mashariki walilolitwaa hivi karibuni na kupata fursa ya kupiga nalo
picha katika viwanja hivyo.

Bendi hiyo inatamba na vibao vyake vipya vya SULUU uliotungwa na
Shabani Dede na NADHILI YA MAPENZI uliotungwa na Juma Katundu.



Habari imeletwa na :
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
       +255774406938
       Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP