Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika mgao wa HESHIMA,.....

>> Monday, August 15, 2011

.....usiye MHESHIMU naye ana WAMUHESHIMUO hata kwa ufikiriayo HAYANA HESHIMA!

Swali:
  • SI chanzo cha MTU kuheshimu MTU kinavigezo visivyofanana ASILI?


Ndio,....
...... kuna ambao MISINGI ya WAHESHIMIWAVYO ni yale usiyoheshimu,...
.... kwa kuwa kwa waliojaribu hayo wanajua katika hayo ,...
......HUYO bingwa!:-(




Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumatatu NJEMA!

Hebu Eve aanzishe upya kwa- Tambourine




Eve aendeleze kwa - Let Me Blow Ya Mind



Au tu BI KIDUDE amalizie tu tena kwa kudai-Ahmada umelewa



3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 3:47 am  

Asante, Mkuu, Mke wangu, LaTsabedze (mwenyeji waSwaziland) ameifurahia moja katika VIDEO zako hizo na kumpenda hasa huyo Bikizee jinsi anavyoimba na jinsi anavyotoa meno yake yale babu kubwa!


Binafsi nasema: Mungu aendelee kukubariki Simon kwa kuendeleza na kutangaza utamaduni waMswahili Mtanzania kwa Msauzi kwa Mkenya na kadhalika pitia nyimbo za Youtube na zinginezo!


Namomba sasa nikunukuu wewe: "...usiye MHESHIMU naye ana WAMUHESHIMUO hata kwa ufikiriayo HAYANA HESHIMA!"



Nakweli, Mkuu!

Mfano mzuri umetupatia wewe mwenyewe kwa huyo Ahmada aliyeanzisha zogo angali bado mtoto kwa wizi wa pombe vichochoroni vya Kenya mwishoe kakua na kuwa mlevi!
(http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=9_dOFaL6XbQ)




Wastaarabu Ahmada bure wanamwonea wivu kwa pombe zake huku wengi wao nao ni walevi kisirisiri. Nayeye kaapa haachi kunywa pombe mpaka...(tena kwa maneno yake kabisa)..."viwanda vifungwe".



Hapo Ahmada ameshajijengea naye sifa na heshima kwa walevi wenzake ingawaje mwanae na mkewe wanakufa njaa kutokana na kutoacha hela kila asubuhi kwa madai yeye sio Benki wala sio ATM!


Na kweli, ulimwengu wa Ahmada si ulimwengu wa mwanamapinduzi na mtetezi wa haki za wanawake na watoto!


Ndio maana mimi binafsi kama Goodman Manyanya Phiri napendelea mfumo wa Nchi Za Magharibi wenye kuheshimu Haki Za Binadamuu kwa kuwa heshima ya Padre na yake Sheikh, KAMWE sisawa na heshima ya mlevi (lakini wote ni binadamu kama Mlevi Ahmada, na wote wakishawekwa kaburini ni kuliwa na funza huyohuyo mmoja!)

Yasinta Ngonyani 11:05 am  

Hehima ni kitu bora sana kuliko "sadaka" Jumatatu njema nawe pia..:-)

Simon Kitururu 12:39 am  

@Mkuu Goodman: Huwa unanifikirisha kweli ukiandika!

Nje ya topiki :
Unajua marakibao nashindwa kukomenti hata kwenye vijiwe vyako(blog ) kisa napotelea kwenye fikiria?

Ila nashukuru Mungu kukufahamu!

@Da Yasinta: Asante mtu wangu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP