Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuna wanunao na HAWAJUI wamenunia nini,....

>> Tuesday, August 30, 2011

.... kama tu kuna WAMCHEKEAO MTU lakini labda ukweli,....
.... ASEMAVYO huyo MTU havichekeshi,...
... hawajui kiwachekeshacho ni nini!:-(

Swali:
  • Unauhakika mtu akianguka wachekao wanauhakika kiwachekeshacho ni ninni?
  • Kwani hujawahi kuamka umenuna na HUNA UHAKIKA na  sababu ikununishayo na unadai tu umeamka vibaya?


Wait aminute,...
..... kumbuka tu ujisikiavyo UKIWA na FURAHA, unahuzuni, unajisikia UMEPENDA eti MWENYEWE limtu fulani,..
....au tu swala la kuwa pamoja na kuwa kuna  MINUSO ya EID wewe husikii njaa,.....
..... jua tu kuwa YOTE ajisikiayo MTU ni matokeo tu ya MAKEMIKALI mwilini yalivyo JIPANGA hata kama hayo utayaita MAHOMONI, tindikali,.....


....au samahani tuangalie MAKEMIKALI kwa ung'eng'e  hata katika mfano wa ni kwanini JIMBWA la POLISI likitokea unaweza kujikuta umetoka BARUTI bado ni mchezo wa kemikali ambao hata ukiutafuta kwenye nukuu hata zile zisizoza  vyanzo vya uhakika sana utakuta wanakusimulia jinsi ni MAKEMIKALI yafanyayo ujisikie kutoka BARUTI au KUBAKI tu chumbani na limtu LILILOKUTISHA na KITU katika ndude ziunganishwazo na ADRENALINE RUSH ikimaanisha :

Adrenaline rush refers to an activity of the adrenal gland in a fight-or-flight response, when it is releasing adrenaline (epinephrine). When releasing adrenaline, one's body releases dopamine and can act as a natural pain killer. A chronic hyper-adrenaline is a common symptom of an anxiety disorder, but in some cases, it may be due to pheochromocytoma, a tumour in the adrenal medulla. An adrenaline rush causes the muscles to perform respiration at an increased rate improving strength. It also works with the nervous system to interpret impulses that trigger selective glands.

Ndio,...
.... kaung'eng'e hapo juu ni kakustua tu jinsi gani ukiogopa mpaka unaogopa tayari kuna mpaka adrenaline  na dopamine katika mfumo wa mwili wako ambazo ni baadhi tu  ya  kemikali vimiminika vigusavyo jinsi unavyo jisikia ingawa kwa undani  swala hili ni la kitabu kizima na sio sentensi moja.

Sasaa :
  •  Si unajua hata ili uote titi  pia ni MAKEMIKALI yanahusika na MWANAMKE  unaweza kumuotesha NDEVU kwa makemikali tu aka HOMONI kama utacheza nazo vyema ?
  • Si unajua kuwa hata hasira, nyege au tu uume wa beberu kudinda yote ni michezo ifanikiswayo na  makemikali ndani ya mwili wa kiumbe hicho?
  • Kwani unafikiri hata hisia zako katika dini hasa zile za ni jinsi gani unaweza kubadilishwa dini kirahisi kuliko wengine hazina uhusiano na UWIANo wa makemikali hata kwenye ubongo wako uwezao kufanya kama yafanyikao kwa wale ambao katika mtongozo ni maji mara moja?


Ndio,...
...... kuna WAKUCHEKEAO bila sababu ,...
..... ingawa pia inawezekana unajua KUCHEKESHA hata kwa kuwa uongeayo ukiwa siriasi ndio KICHEKESHO kama unashangazwa na wachekao wakati wewe uko siriasi!:-(



Na ndio,...
.... ni makemikali MWILINI mwa MTU yasaidiayo kufanya anayependa ajisikie anavyojisikia AKIPENDA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala USIKONDE!:-(



Hebu Offside Trick na Hammer Q warudishe -Dege




Franco na T.P. OK Jazz waingilie kati kidogo kwa-Simba Nkoni



Eddie Murphy na Shabba Ranks waingilie nakubadili muelekeo wa mchezo mzima kwa- I Was A King



Shabba Ranks na KRS One wabadilishe muelekeo zaidi kwa - The Jam



Au tu KRS 1 amalizie tu kwa -Sound of da police

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 7:39 pm  

Kweli kabisa MTAKATIFU.

Simon Kitururu 8:27 am  

@EDNA: Asante kwa kunitembelea ! Ulipotea kidogo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP