Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kasirika MDAU sasa hivi kama una HASIRA na chekelea kama unakikuchekeshacho!

>> Friday, August 19, 2011

Ndio,...
....labda kuna sababu BINADAMU ameumbwa na uwezo wa kupandwa HASIRA,...
..... na labda kama hucheki wakati unakikuchekeshacho,...
.....unajinyima DAWA ya bure MAISHANI.

Swali:
  • SI unajua kuna madhara ya kutunza hasira na unaweza ukawa unajitengenezea mazingira ya kukasirikia WASIOHUSIKA?
  • Na si unajua KICHEKO ni DAWA?


Ndio,...
.... inasemekana kuna maeneo kama msibani KUCHEKA kisa mtu kajamba labda ni tabia mbaya,...
..... lakini KUJIBARAGUZA hucheki wakati umechekeshwa labda ni UNAFIKI,...

Na kama unatunza HASIRA ambazo misingi yake ni KAZINI na umezitunza kwa kutoonyesha hasira hukohuko kazini ,...
... usije kujishangaa ukizihamishia HASIRA za ofisini kwa wafanyakazi wenzako nyumbani kwa watu wasiohusika.


Swali:
  • Kwa hujawahi kusikia hata MWALIMU aliyechukizwa nyumbani labda hata kwa kunyimwa tu unyumba anaweza akawa mkali bila sababu kwa wanafunzi darasani?
  • SI nasikia bosi aliyekasirishwa nyumbani huwa anamchezo wakuwa mkali kazini?

Ndio MDAU,...
..... katika vyakutunza labda sio HASIRA,...
....na  kama unachakucheka sasa hivi cheka kwa kuwa hatujui kesho itakuja na vidubwana gani!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ijumaa NJEMA!


Hebu Oliver N'GOMA aanzishe upya kwa - Ngé



Oliver N'goma na Bhonos warudie pia -Alphonsine



AU tu Oliver N'goma amalizie na -Julie

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:58 am  

kweli HASIRA HASARA..IJUMAA NJEMA NAWE PIA Simon.

Simon Kitururu 6:42 pm  

Ijumaa njema Kapulya!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP