Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukiangalia UCHOYO wa MAWAZO ya Binti KHALUFANI katika KUNYIMA watu ANACHOFIKIRIA na wala sio MWILI!:-(

>> Monday, August 08, 2011

Kuna ambao wako KIMWILI,...
.... ila KIFIKIRA hawapo hapo ,...
......na waliopembeni yao wanabunia tu nini kipo MAWAZONI mwao.

Swali:
  • Unabisha?


Aliyeko pembeni yako angekuwa anafikiria kwa SAUTI hata kabla HUJAMCHEKEA,...
.....labda kuna anachofikiria ambacho hujawahi kukifikiria ,...
.... ambacho ni una sura nzuri na labda unafaa KUBAKWA!:-(

Swali:
  • SI unajua labda sio lazima tunajua UNAFIKIRIA nini hasa ukiwa KIMYA?

Ndio,...
.... labda SEMA ufikiriacho,...
..... kama nia ni tujue hata yale mambo madogomadogo kama ya kuwa unapenda MAGIMBI kuliko VIAZI vitamu.:-(

Swali:
  • Si labda kutegemea watu wastukie tu UNAWAZA nini ni kuonea watu wengine ?
  • Na si unajua labda FIKIRA zako ndio zenye MAJIBU na kukaa kwako kimya na fikira zako labda ni aina moja wapo ya UCHOYO?
  • SI unajua kuna wengi ambao wanaweza kukupa mwili ila hawakupi NG'O wanawaza/WANAFIKIRIA nini? 
  • Na si unajua labda ungejua RAFIKI yako anawaza nini labda huyo angegeuka kuwa ADUI yako?

Ndio,...
.... labda kutulia na MAWAZO yako ni aina ya UCHOYO,...
.... ingawa kuna uwezekano MTU kutulia na mawazo yake ni chanzo cha kupata MSONGO wa mawazo kitu ambacho kiafya za akili labda huzaa UGONJWA!:-(

Swali:
  • AU?

Ingawa  labda,...
.... ASANTE MHESHIMIWA kwa kukaa kimya maana ungesema unachofikiria,....
..... labda bonge la PILAU lingeanza kutia kichefuchefu watu kisa unavyolifikiria tu kimatapishi!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
JUMATATU NJEMA!





Hebu East African Melody warudie-Utalijua jiji




Tubadili tena kwa kukatizia tena UGANDA ili Moses Radio & Weasel warudie-Ring a Bell



Au tu Radio &Weasel waendelee kutubakiza hapa UGANDA kwa -Talk and Talk aka TOKO TOKO


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

hansom 2:28 pm  

Hivyo kwa wale wanaosema wnajua unawaza nini wanadanganya!? Kwani wanaweza kukuambia unawaza kupata nguna(ugali) ndondo, lakini ukasema hawajapatia kwa vile unajua itakuwa aibu kwako kwa vile una njaa, ingawa kweli unawaza nguna, ni mawazo yangu tu ninayowaza ingawa huwezi amini kuwa nawaza hivyo kwa sasa mkuu!!

Yasinta Ngonyani 3:55 pm  

Ni jumatatu na hili wazo ni lenyewe:-) tupo pamoja niwuyili!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP