Je, unajua Kila unapofungua website au blog unaacha fingerprints? Ina madhara hivyo jifunnze kujihami
>> Friday, September 02, 2011
Huwezi kutumia internet kwa matumizi ya kawaida bila kutumia Internet browser. Hii ni interface inayotuwezesha kufungua blog, websites na progams nyingine za Internet. Kuna aina sita za Internet browser:
Internet Explorer – Microsoft Inc
Google Chrome – Google Inc
Mozilla Firefox – Mozilla Corporation
Safari – Apple
Opera – Opera Software
Netscape – Netscape Communication Corporation
Ili kurahisisha matumizi yake, Internet browser zote zinahifadhi kumbukumbu ya web sites zote ulizotembelea. Zinafanya hivyo kwa sababu kadhaa. Sababu ya kwanza ni kwamba kwa kuhifadhi kumbukumbu hizo huwa inamrahisishia mtumiaji anapotaka kutembelea website hizo hizo hapo baadaye. Hii inapelekea internet experience kuwa faster kwa sababu baadhi ya information imehifadhiwa kwenye komputa yako na sio kwenye server maili kadhaa kutoka ulipo.
Pamoja na kwamba web browser inaokoa muda wako, kuna mswala kadhaa yanayoweza kuleta madhara kwenye komputa yako.
Kwanza kumbuka kwa kuwa wewe umerahisishiwa unapotembelea web sites ulizozoea, hali hii inamwezesha mtu mwingine kuziona kumbukumbu hizo zinazohifadhiwa na web browser. Baadhi ya web site ulizotembelea inawezekana information zilizohifadhiwa ni muhimu au za siri (kama mambo ya kikazi). Mtu mwingine mwenye nia mbaya anaweza kujua kila website uliyotembelea na nini ulichofanya kwenye website hiyo. Kuepusha watu kuona information zako usiache fingerprint unapotumia internet. Unafanya hivyo kwa kufuta (delete) kumbukumbu zote ambazo web browser imazihifadhi.
Unaweza kufuta kumbukumbu hizo kirahisi kabisa kama ifuatavyo:
Google Chrome: Select “Tools” and choose “Clear Browsing History”
Safari: Click on the “History” tab in your menu bar. Select “Clear History” located at the bottom of the list.
Internet Explorer: Select the “Safety” drop down menu at the top right of the screen. Choose “Delete Browsing History.”
Mozilla Firefox: Click on the “Tools” menu, then select “Clear Recent History.”
Pia kuna njia nyingine unayoweza kutumia web browser bila kuacha fingerprint. Web browser zote zina feature inayokuwezesha kufanya hivyo: Kwa watumiaji wa Internet explore hii inaitwa “In Private”; kwa Mozilla Firefox na Safari hii inaitwa “Private Browsing”; na kwa Google Chrome hii inaitwa “incognito”. Njia hii ni nzuri zaidi hasa kwa wale wanaotumia komputa za public kwa mfano cafĂ©, shuleni, vyuoni, kazini, n.k.
Soma zaidi tembelea blog yako ya teknolojia hapa : http://it4dev.blogspot.com/
Kila la kheri!
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ahsante kwa taarifa!
Post a Comment