Wakati kuna umuhimu wa KUFIKIRIA wengine WANAVYOKUFIKIRIA,....
>> Thursday, September 08, 2011
.... umekumbuka kustukia ni kivipi UNAKWAMISHWA kwa kufikiria,...
..... wengine wanakufikiriaje?
Ndio,...
..... kuna waathirikao zaidi ya MAVAZI na MITINDO ya nywele,....
...... kwa kuwaza tu WENGINE wanawafikiriaje kitu kifanyacho wanashindwa kuwa WAO mpaka ya zaidi ya kujikuta wanalazimika kuchambia TISHU iliyo MAARUFU huku wakiamini MAJI maliwatoni ndiyo yanaweza zaidi shughuli za kimakokoneo.!:-(
Swali:
- SI kuna wakwepao kuvaa midabwada waipendayo kisa wanaogopa wataonekana MASIKINI?
- Na sinasikia kuna ambao mpaka hukwepa kuonekana na WAPENZI wao kwa kuhofia wengine watafikiria nini hasa kwa kuwa wanaaamini WAPENZI wao wana meno kama ngiri wakati wakiwa na KICHWA kama mende?
Ndio,...
...... labda kumbuka tu labda wengine WAFIKIRIAVYO,...
....... sio muhimu sana kwa kuwa hilo ni jambo lao na kila MWENYE BICHWA hataufanyeje huwezi kudhibiti AWAZACHO.
Swali:
- Si unakumbuka kila MTU anamchezo wa kufa kivyake na yake kitu kifanyacho labda ya wengine ni MZUGO tu katika maisha haya ambayo KIAINA hatusaidiani kufa?
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Hebu EDDIE MURPHY aanzishe tena,....
Au tu Kool & The Gang waingilie kati kwa - Fresh
Kool & The Gang waongezee dozi kwa-Cherish
Kool & The Gang wadinye - Get Down On It
Kabla hawajamalizia kwa-Celebration
11 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Duh! ingewezekana kumfungua mtu na kuona ni jinsi gani anamuwaza mtu mwingine ingekuwa afadhali:-) nimekipenda kicha cha HABARI PIA ULICHOANDIKA.
@Yasinta: Ingekuwa inawezekana kumfungua mtu ili kuona ni jinsi gani anamuwaza mtu mwingine labda ungestukia mie mmeo kisiri!:-)
Ila kuna rafiki yangu yeye anaamini labda tungekuwa hatuwazi tena kama binadamu angekuwa anajua tu kitu kiendeleacho kichwani mwa mtu mwingine!
Unafikiri MUNGU anawaza?
Wow! Ingekuwa bomba la jambo...kustukia hilo:-) Mimi nina imani Mungu anaweza Simon
Doh!,nimemisi, mijadla kama mitatu hivi kutoka kwako,mtakatifu.nimeicheki nikaona basitu haikuwa ridhiki yangu nichangie,sasa sijuwi ndo kufikiria wengine wanavyoku fikiria usipo sema chochote kwenye blog ya mtakatifu.anyway kitu kimetulia ngoja kwanza nimalize kupika. kaka S.
kaka S. wala hujachelewa..unapika kila wakati ..unapika nini leo?..ooh samahani nimetoka nje ya mada ...Fikiria
Simon kuna ujumbe wako kweny add ya barua pepe yako angalia tafadhali!!
Hili ni tatizo kubwa na linaweza kukukwamisha mtu usiendelee. Matineja wengi leo huishia kuvuta bangi au kutumia madawa na hata kungonoka kihatarihatari wakiogopa kwamba wataonwa kihasi na washikaji zao. Na hata mijitu mizima utakuta inajibidisha kuonekana isivyo eti ikihofia kufikiriwa kuwa imefulia!
Kama Mungu Anawaza, hata mimi ningependa kujua anawaza nini na wakati Yeye Anajua kila kitu.
Inawezekana Anawaza kwani siamini kama Aliamka tu siku moja na kuiumba dunia bila kufikiria kwanza. Au pengine tunawaza kibinadamu wakati Mungu "Anawaza" kivyakevyake.
Ati, ni lazima kuwaza???
Kaka Matondo...hapo hakika umenena kuhusu watu wanavyojibadili na kufikia hatua hiyo...kwa kweli ni hatari sana na wengine wanakuwa wanajifikiria na mwisho huamua kutoa maisha....Kuwaza/kufikiri nadhani ni muhimu lakini kuna wakti mtu unaweza ukafanya jambo bila kufikiri na baadaye ukafikiri....
Ni vema sana kuwafikiria wengine wanawaza nini. Hiyo ni afya ya kiroho kama vile maji ni afya ya kimwili.
Lakini maji yakizidi utazama tu; na ukiwa unawawaza wengine kiasi cha kuogopa kutoka nje kwa kuwa umevaa kiraka chako, basi LAZIMA UMUONE mganga wa akili aisee... sio utani!!!!
Mkuu niajiiba iba kutizama , lakini nachungwa kama mfungwa, nchi hii sasa nikama tupo utumwani,....wakati wengine wanaingia dunia mpya sisi tunapigwa vita...!
@Da Yasinta: Nimeusoma ujumbe ingawa nimechelewa! Ntaufanyia kazi!
@Kaka S: Wala hujachelewa Mkuu!
@MKuu M.M.N:Mie nahisi KIBINADAMU ni lazima KUWAZA tatizo hujitokeza tu pale katika``TUNAWAZA NINI!´´:-(
Kuhusu ya MUNGU labda siri zake anajua MUNGU MWENYEWE yani!
@Mkuu GOODMAN:Hapo umenena Mkuu!
@Mkku M3: Tuko Pamoja Mkuu!Tutafika tu!
Post a Comment