Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati SIRI ya KUJIHAMI na KUPWAYA KWA KUBWA labda ni HISIA TU za kuwa NANILII NDOGO haziumizi !

>> Friday, September 02, 2011

 Na hisia ndizo zifanyazo MPAKA  kunawajihamio na  kutangaza hawajaachia ushuzi,...
.... kitu ambacho ni kweli kuwa sio wao walioachia ushuzi,....
.... kwa kuhisi tu labda WATU wanafikiria ni wao waliochafua HALI ya HEWA!:-(

Swali:
  • NI mara ngapi  WEWE MWENYEWE UMESHUHUDIA watu wahisivyo huwa  SIVYO?
  • Unauhakika SINDANO NDOGO haiumizi kwa muogopa SINDANO?
  • Na unafikiri kujihami huondoa UMIVU kama UMIVU lipo tayari?

Na kujihami labda sio SULUHISHO,....
..... kwa kuwa mara nyingi anayejihami huwa napoteza tu nguvu kwa kuwa angetulia angestukia katika ndude LABDA suluhisho halikuhitaji kitendo cha KUJIHAMI!

Swali:
  • SI inasemekana anayejihami hutumia nguvu sana zaidi ya hata aliyetulia na kukabili swala kiutulivu?
  • Na si ukijiandaa hauhitaji KUJIHAMI?

Ndio,...
.... hisia BINADAMU tumeumbwa nazo kwa kuwa ni muhimu,....
...... na KUJIHAMI tunauwezohuo kwa kuwa kuna umuhimu wake pia,....
..... lakini kumbuka tu si kila uwezo alionao BINADAMU inamaana autumie kila awezavyo na labda ndio maana hatuendi choo popote tu pale sie kama BINADAMU kisa tumehisi tu shehena ya CHOO inapiga hodi na uwezo wa kwenda choo hata kama ni KIHAJA KUBWA  tunao!:-(


Swali:
  • AU?

Na kujihami na KUBWA,...
..... labda tuanzie katika kujiuliza ni nini kimetufanya tutambue jambo kama KUBWA,...
.... kwa kuwa mara nyingi labda UKUBWA wa KITU  umepotoshwa tu na TULIVYOJIFUNZA mambo na ndio maana hata MAGONJWA makubwa ukubwa wake uko kwenye virusi vidogo hata bila DARUBINI havionekani.

Swali:
  • Unabisha?



Ndio,....
....kikujihami  kubwa zima linaweza kuogopa MENDE MKUBWA  kuliko vijidudu vya UKIMWI visivyoonekana hata kwa macho kwa udogo,....
..... kwa kuwa KIHISIA anaogopa alilojifunza kuwa KUBWA ,....
.... wakati kiukubwa wa halihalisi  VIJIRUSI vidogo kama vya UKIMWI mende na misuli yake HAONI ndani!:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA!



Hebu MANU DIBANGO aanzishe upya kwa -SOUL POWER





Manu Dibango angizie tena-Woa





Manu Dibango amwage na - Cadence moi Ca



Manu DIBANGO adinye -Pepe Soup



Au tu Manu Dibango aje tena na Courtney Pine warudie - Aye Africa





Kabla hajachenji gia na kumwaga-Africafunk



Halafu anyunyizie-PATA PATA




Halafu kwa leo amalizie tu  na - Soul Makossa







2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:59 am  

Ahsante kwa wazo la ijumaa ya leo kuna kitu nimejifunza ..n...basi naacha...ijumaa njema nawe pia!

Simon Kitururu 9:17 am  

Asante Kimwana Yasinta!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP