Ya WENGINE yangekuwa YANGU!
>> Friday, September 02, 2011
Ningekuwa na BONGE la NYUMBA!
Ningeendesha bonge la GARI!
Ningekuwa na bonge la MPENZI!
Ningependwa kama FULANI!
Ningefuata DINI na mbinguni watu wangedai ntaenda kama FULANI!
Ningesaidia NDUGU , jamaa na MARAFIKI bila kuruka watoto wa mitaani kama FULANI!
Ningekuwa huru kuwa malaya na mwenye kujiamini kama FULANI!
Ningekuwa napata minofu ya nyama mikubwa kama BABA mezani!
Swali:
- Umestukia lakini mara kibao MTU uwezavyo kusahau kuwa utamanivyo ya wenzako labda kuna watu kibao watamanio YAKO?
Lakini,...
.... kwa kuwa SIE ni SIE na SIE sio WATU wengine,...
..... labda tujifunze kustukia na baraka tulizonazo hata kama tulipo CHAMOTO TUNAKIONA!:-(
NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Hebu twende tena Brazil ili Gilberto Gil aanzishe upya kwa -Aquele Abraço
Aje tu live tena na ndude hiihiii,...
Au tu ghafla tu Angelique Kidjo abadili mchezo kwa ~Afia
Kabla hajamalizia kwa kurudia-Wewe
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Umesema kweli kabisa kaka Simon turidhike/tufurahi na tulivyonavyo na kama tulivyo. Ila hili lazima niseme ningeweza kuwaza kama wewe ninge....au labda nisema ungekuwa kaka yangu yaani si wa hiari ningejivuna zaidi ya ninavyojivuna sasa:-) Jioni njema Simon
Nimekupata, weekend njema Mkuu
Pigo la Mjeledi Huchapa Ngozi, Lakini Pigo la Ulimi Laweza Vunja Mifupa. Bora Kufa Ktk Fikra Zinazoishi, Kuliko Kuishi Katika Fikra Zilizokufa.
Asante Yasinta!
Wikiendi njema kwako pia Mkuu CHIB!
FIkira zilizokufa ni zipi hizo?@Rasta Mcharia!
@Simon kwa niaba ya Mcharia
Imani nzuri ya mtu haifi kamwe naye, kwani wapo wengine watakayoindeleza baada ya kifo chake na ndio maana hadi leo tunao mawazoni akina Karl Marx, Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Yesu Kristu, Buddha, Musa, Mohammed, Pixley Seme na wengine watakatifu.
Kuhusu mandhari ya leo, Mkuu: SAFI SANA!!! Lakini utajiri ni kitu rahisi sana. Amua mwaka ujao mzima kumwabudu shetani na utapata vyote tu!
Lakini nami nikiwa Manyanya ninazo tamaa zangu kibao; na moja yake ni kusikia siku moja wimbo wake Angelique Kidjo akifanya DUET na Celine Dion. Wafikiri wimbo huo utakuweje sikioni, Mtakatifu Simon? Sawasawa na wimbo wa malaika wawili?
@Mkuu PHIRI: Hiyo kolabo ya Angelique na CELINE itakuwa matata sana yani! Miezi miwili iliyopita nilifanikiwa kumuona live akiwa katika mradi wauitaoSING THE TRUTH ambapo Angelique, mdada muimba INJILI aitwaye LIZZ Wright na mdada mwingine aitwaye Diana Reeves ndio walikuwa kundi moja katika kuwakilisha sauti. Nilikoma mwenyewe. Baada yao akaja Elton John nikashindwa kumsikiliza kwa kuwa mahitaji yangu yalishatimizwa na malaika hao!:-(
Post a Comment