Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BADO labda ni kweli kuwa STAILI ya MHESHIMIWA ya kutokea GESTI BUBU na MKE wa MTU,....

>> Monday, May 16, 2011

.... inaegemea zaidi katika silaha iitwayo KUJIBARAGUZA,...
.... na wakati huo MHESHIMIWA afanyacho ni KUJIBARAGUZA kuwa hajatokea GESTI hiyo na MKE wa MTU!:-(

Na KUJIBARAGUZA ingawa ni silaha nzuri  iletayo uhaueni kama  MTU anasikia choo kuhusishwa na kijambo chake HADHARANI na swala hilo likafanya ajifanye hausiki na uchafuzi wa hali ya hewa katika sebule hiyo ugenini kwa KUJIBARAGUZA,...
.....lakini  bado yasemekana KUJIBARAGUZA kunaweza KUPONZA mtu PIA  kwa kuwa kunaweza kusababisha MASIKINI  ajibaraguze  kuwa ni TAJIRI kitu  ambacho  huweza kumuharibia MASIKINI mpaka  BAJETI ya unga wa MIHOGO  na MATEMBELE kwa kuwa  KUJIBARAGUZA kuna mchezo wa kujifanya yako sio yako na wewe ni mwingine MTU!:-(

Swali:
  • Unakumbuka mara ya mwisho ulipojibaraguza kuwa HUHUSIKI wakati  labda UNAHUSIKA TU hata katika swala la kwanini TANZANIA inajulikana kama NCHI masikini?


Ndio,...
... ngojea nijibaraguze kuwa aliyeandika hapa sio MIMI!:-(


Ndio,...
.... hili ni wazo tu MHESHIMIWA na LABDA wala usikondeshwe na hii TARALILA!:-(


Hebu Juliana Kanyomozi na KIDUMU waanzishe upya kwa-Haturudi NYUMA



Halafu hebu DIAMOND aturudishe - MBAGALA



Au tu MATONYA arudishe pia swala la -Spea TAIRI



Kabla huyuhuyu  MATONYA hajahamishia hoja kwenda kwenye-Taxi BUBU

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:14 pm  

Mapenzi yana nguvu kuliko mauti. au pia....mmhh nimesahau kidogo ngoja ninywe kwanza chai yangu isiyo na sukari huwa inanikumbusha...

Simon Kitururu 3:07 pm  

@Yasinta: Kumbe umestukia eeh!


Nasubiri kwa hamu kikombe chako cha chai kiishe ili uje tena kutufundisha kuhusu mapenzi mtu wangu!

Yasinta Ngonyani 5:06 pm  

Mapenzi...kipenda roho hula nyama mbichi...Mapenzi yanaweza yakamfanya mtu apagawe. Lakini hivi ni kweli mtu unaweza ukawapenda wanawake/wanaume wangapi? ....mmmhh nahisi...ngoja niache isije nikachanganya mada hapa!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP