Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunajiuliza kama MWIZI huwa ni kweli anakuwaga na HAMU ya KUIBA!

>> Monday, May 16, 2011

HAMU ya kitu ni kitu cha ajabu,...
.... ila:

  • Je unafikiri MUONGO huwa anahamu ya KUDANGANYA na malaya huwa na hamu ya umalaya au yote ni matokeo tu ya mtiririko wa yajiletayo mbele ya MTU kiuwezekano?

  • SI mambo mengi ufanyikaji wake hutokana na uwezekano unaojianika mbele za MTU kitu kifanyacho waliopo kwenye MAKANISA ya KIKATOLIKI ni rahisi kujikuta ni WAKATOLIKI kwa kuwa hilo linawezekana?

Ndio,...
.... labda hata MWIZI labda huiba kama tu inawezekana,....
.... na labda huwa wala hana hamu ya kuwa MWIZI!:-(

Swali:
  • SI inasemekana MAFISADI wengi hawakuzaliwa mafisadi na huwa MAFISADI tu pale wakiwa kwenye OFISI inayowezesha wao kufisadi kitu na kufanya tendo hilo kuwa ni liwezekanalo?

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumatatu NJEMA!


Hebu Eric WAINAINA na OLIVER Mtukudzi waanzishe upya kwa- Twende Twende






Eric Wainaina aendeleze tu kwa -DUNIA ina MAMBO



Au tu MARIJANI RAJAB arudie wimbo-Ewe KIJANA

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 9:25 am  

Ni kweli , wakati mwingine mtu anafanya kwa `udhaifu fulani' na matokeo yake hujuta, na wengine wakionja asli ndio basi tena.
Ki-imani tunasema watu hufanya mabaya kwa nguvu za shetani au ibilisi...au sio?

Simon Kitururu 10:33 am  

@M3: Ndio Hapooo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP