Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunaangalia tofauti ya KUCHACHA kwa CHANGUDOA mwenye BAJETI na MIPANGO na KUCHACHA kwa asiye na BAJETI yenye MPANGO!

>> Tuesday, May 10, 2011

Kuchacha kwa mwenye BAJETI na MIPANGO,....
.... hakumaanishi  aliyechacha akaunti yake  iko TUPU,...
..... kwa kuwa WENYE mipango na kujua KUBAJETI,....
..... usishangae wakijinyima wakati  wana MILIONI kwenye AKAUNTI hasa kwa kuwa KIMIPANGO watakachokufanya  kinahitaji wawe na MILIONI MBILI na zaidi!

Swali:
  • SI umestukia  kuwa kwa wasio na MIPANGO na wasiofanya BAJETI huweza kujisikia hawajachacha kwa kuwa wanaona akaunti ina hela ?

Tukiacha utani/STORI YA KWELI:

Moja ya kitu nilichojifunza baada ya kutoka nyumbani na kwenda shule ya bweni enzi hizo MAZENGO sekondari DODOMA  ilikuwa ni kuwa na BAJETI na MIPANGO.

Nakumbuka  naingia  kidato cha tano pale DODOMA nikijisikia ahueni kabisa kwa kuwa nilijitahidi kupiga mizinga ya NGAWIRA PESA  kwa kila niliyemfikiria kitu  ambacho kikafanya nijisikie kuwa naenda shule nikiwa na fweza za kutosha mpaka likizo itakayofuata.

Basi bwana nikaingia DODOMA  moja kwa moja bweni la MWENGE pale mazengo. Jioni ilipofika ikawa ndio kwa mara ya kwanza inatakiwa nionje chakula cha shule. Basi baada ya kwenda  bwaloni kucheki msosi, nikakuta huko kuna UGALI mbaya kama nini na maharage ambayo ni kama yamechemshwa tu na maji bila mafuta wala chumvi au viumngo vyovyote vile. Basi kilichonijia akilini ni kuwa mie siwezi kula msosi huo kwakuwa NA PESA  na nikakumbuka kuna mtu alishanitonya kuwa kuna wauza machapati , vitumbua  maandazi nk wajao karibu na MABWENI -  kwa hiyo moja kwa moja nikaamua naenda kununua machapati na vitumbua kwa kuwa mie sipendi maandazi na kugeuza hicho kuwa ni msosi wangu  kwa chai ya maziwa. Unajua tena nilienda shule na maziwa ya unga na vikorombwezo vingine.

Basi hiyo ikawa ndio tabia. Asubuhi mchana jioni  mambo yote ni kujinunulia vyakula na siku  nikiwa na nafasi naenda mpaka kutafuta Dodoma wine ili kushushia  shughuli. Na kumbuka kwa kuwa DODOMA maji yake ni ya chumvi basi ilikuwa ni fulu kununua maji ya chupa na maji ya DODOMA ilikuwa ni kwa ajili ya kuogea tu!

Basi bwana kama mtu ambaye hakuwahi kujipangia bajeti hata siku moja kabla ya kwenda kidato cha tano unaweza kustukia kilitokea nini baada ya muda  enzi hizo ambazo ndio kwanza nabikiri  akaunti ya benki ya posta. Siku moja ikatokea najisachi na kustukia sina keshi na  nacheki kitabu changu  cha benki nastukia duh pesa iliyobakia  wiki haiishi na hapo wala hata likizo hainukiii kufika.

Wacha nikune kichwa na taratibu kujikuta naanza kula ugali wa shule na maharage hayohayo niliyojifanya nayakimbia mwanzoni. Maji ya chumvichumvi ya DODOMA yakageuka matamu tu. Chapati na vitumbua vikageuka vitu vya lakshari. Nikajifunza ukichacha vizuri  na unanjaa msosi wowote unalika aisee.  Baada ya mshtuko wa kwanza huo nikagundua kuwa ukikiona kiburungutu na hujakipangia mkakati labda hicho wala sio kiburungutu kihivyo.  NA NI MARA YA KWANZA ndio nikajua KUCHACHA kupo hata kama UNAPESA na kinachoweza kutokukustua kuwa umechacha  ni UDHAIFU wako wa KUBAJETI na pia kukosa kwako MIPANGO ya nini unataka kufanikisha.


Na baada ya kuanza kuishi zaidi nje ya TANZANIA zaidi ya TANZANIA ambako hata serikali yake inamatatizo ya KIBAJETI nikazidi kufunzwa hili jambo hasa baada ya kukutana na watu wanajinyima kama nini na kuonekana kama wanateseka kabisa  wakidai hawana pesa,...
... halafu baadaye WANAKUSHANGAZA  kama alivyowahi kunishangaza RAFIKI yangu MMOJA ambaye NILIAMINI KACHACHA  baada ya kuniaga eeh bwana ee mie  kwa miezi mitatu ijayo nazunguka dunia nisha pata viza za nchi kadhaa wa kadhaa na  nahangaikia tu  ya North Korea sijui nitaipa au vipi. Mie nauliza wewe si siku zote hizi ulidai umechacha na unateseka kinamna?  Jibu nililopata lilinifungua sana macho kuwa ile kuchacha ili kuwa ni kwasababu ya mipango na BAJETI vilikuwa havijawiana kwa kuwa jamaa nia yake ni kuzunguka dunia kitu kimfanyacho anakula mlo mmoja   nakadhalika na kujinyima kisawasawa.

Unaweza kuniuliza ni kwanini nimeandika TARARILA hii!

Ukweli ni kwamba mie naamini sie WATANZANIA hatuna ujuzi sana wa KUBAJETI na mpaka SERIKALI yetu inatatizo hilohilo.

Na naamini mpaka neno KUCHACHA  kwa MBONGO maana yake ni kuwa huna kabisa pesa wakati wenzetu hisia zao za KUCHACHA wanakuwa nazo hasa kutokana na MIPANGO waliyonayo. Kwa hiyo unaweza kukuta mtu ambaye ukijifananisha naye unadhani ni tajiri wakati yeye anaamini KACHACHA.


Labda ingekuwa bomba kama sisi WATANZANIA tungejifunza pia KUCHACHA  kutokana na MIPANGO  tuliyo nayo na pia kujifunza kuwa kama una vipesa kwenye akaunti yako BENKI labda bado umechacha kama hivyo havikusaidii kutimiza MIPANGO YAKO!:-(




Swali:
  • Si labda ni kweli  MBONGO akikuambia kachacha na MJERUMANI akikuambia KACHACHA wanaweza wasiwe wanaongelea kitu kimoja?

  • Na si inawezekana serikali ya MAREKANI iongeleavyo KUCHACHA na kudaiwa na serikali ya TANZANIA iongeleavyo KUCHACHA na kudaiwa wanaongelea vitu viwili tofauti na ndio maana serikali ya MAREKANI wakati  huu isemekanavyo kuwa imechacha bado unaweza kusikia  IMETOA misaada Tanzania ingaw labda misaada yao ni moja ya kitega uchumi ?
Ndio,...
.... labda KUCHACHA ,...
.... kuna aina tofautitofauti zake PIA!:-(



Na hili ni wazo tu la JUMANNE Mheshimiwa na wala usikonde!:-(

Hebu Zap Mama aongelee-Africa &; art




ZAP MAMA aingie kazini-Bandy Bandy



ZAP MAMA atwange-Poetry Man


Au amalizie tu tena na -Sweetie Melodie

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP