Leo katika UCHOKOZI: Tatizo AFRIKA sio DINI za KIGENI ukizingatia UKRISTO ULAYA ni DINI ya KIGENI ukiachilia mbali kuwa Wazungu walipoletewa UKRISTO walimbadili YESU kuwa MWEUPE PEE na MWENYE MACHO ya BLUU ili awe MZUNGU MWENZAO ,....
>> Friday, May 27, 2011
.... kitu ambacho ,...
....LABDA NDIO SIRI ya MAFANIKIO ya KUIGA ya WATU kwa mafanikio,....
.... na waliposhindwa kumfanya Mtume MOHAMMED (s.a.w)kuwa MZUNGU kama WAO wakafukuzilia mbali UISLAMU,......... kitu ambacho,...
.....LABDA NDIO SIRI ya MAFANIKIO katika VISIVYOIGIKA kwa mafanikio yabidi VIFUKUZILIWE mbali!:-(
Swali:
- AU?
Labda ni kweli kama unaiga basi fanya UIGAVYO viwe vyako KIVYAKO kama walivyofanya WAZUNGU kwenye UKRISTO walioutoa MIDO ISTI/Mitaa ya fulu kubwengana WAARABU na WAYAHUDI kwa waarabu na WAYAHUDI ,...
....au kama WAJAPANI walivyofanya na MATEKINOLOJIA ya WAZUNGU kuanzia kwenye MAGARI mpaka nanihii ambacho ndicho CHINA ifanyacho sasa hivi,....
... au kama wafanyavyo URUSI baada ya kustukia UKOMONISTI mambo zake valuvalu kitu ambacho NYERERE alistukia mapema na KUNG'ATUKA katika maswala ya KIJAMAA!:-(
Swali:
- Hivi unafikiri UBEPARI haujatushinda bado TANZANIA kwenye nchi ambayo hata sheria zetu bado ni za MUINGEREZA na wajanja ni waliosoma vitabu visivyo na asili ya TANZANIA?
- Kwani hufikiri moja ya sababu AFRIKA dini za watu zinatuzingua labda ni kwa sababu bado YESU wetu aka NABII ISSA bado ni MZUNGU na Mtume MOHAMEDI (s.a.w) bado ni MUARABU?
Ndio,...
... labda TATIZO la UIGAJI wa KIAFRIKA bado haujafikia kugeuza tuigavyo viwe vyetu KIVYETU,...
....kuanzia kwenye mambo ya DINI ambazo yanatugombanisha SISI kwa SISI,....... mifumo ya UONGOZI , siasa na UCHUMI ambayo bado hata kwa lugha za kikwetu bado twashindwa kuielezea kwa wananchi wetu na AJUAYE zaidi ni yule aliyesomea NJE na asifiwaye na PROFESA wa nje ambaye hahusiki na maisha ya KILA SIKU ya MUAFRIKA hapa AFRIKA,....
..... na yasemekana mpaka hata katika maswala yale ya chupi pia bado chupi bora ni za nje.:-(
Swali:
- Unabisha?
Ndio,...
....labda AFRIKA tatizo sio DINI za KIGENI,...
.....mifumo ya utawala ya kigeni , ....
....mifumo ya uchumi MPAKA hata demokrasia zenye kifafa za nje ...
...... kama tungekuwa tunamkakati maalumu wa jinsi ya KUIGA na kugeuza tuyaigayo yawe YETU KIVYETU!:-(NI UCHOKOZI TU huuu na ni WAZO TU HILI MHESHIMIWA,...
... na HAKI YA NANI TENA wala usibanwe chupi!:-(
Hebu tubadili wazo kwa kumdeku BABA naye akinyonyesha- kwani nanikasema wanaume hawana matiti?:-(
Turudi tu ghafla MADAGASCAR ili DADAH adinye- Madimozely
Au ngojea tubakie kidogo tu zaidi hapa Madagascar ili KIAM'BE adinye pia na - Mavandy
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mmmmh
Tatizo, ni nini, kuiga au `umasikini'
Unajua kuna jamaa kaniambia kuwa uliwa masikini kila cha tajiri utakiona ni kizuri hata `mavi' yake...nilicheka kusikia hivyo...ni kwelii hilo nenokalitamka hivyo, `mavi' lakini lina maana ndefu ukilitafakari...hebu angalia tunayoiga sasa hivi, wenzetu walishayafanya kinyesi,...au tuseme mavi, sisi twayaona bora!
Ni hayo tu mkuu kwa nyongeza TUPO PAMOJA, NA USISAHAU TUMEKARIBISHWA MAKANDE KWA DADA YASINTA!
@Edna: Mmmh!
@M3: Mimi nahisi tatizo sio kuiga bali ni``JINSI gani MTU anaiga!´´:-(
Umasikini na UTAJIRI nafikiri siomuhimu sana katika swala la KUIGA,...
....ndio maana utakuta kuna MATAJIRI walifikia kuchana mpaka MA-JEANS yao magotini na mpaka kwenye makalio kwa kuiga MASIKINI halafu ikaitwa kuwa ni FASHENI ambayo matajiri mpaka kama akina MADONA walishavyaa majinsi yenye viraka na kuchanikachanika.
Na nimekaribia MAKANDE kule kwa YASINTA ingawa naona kwao PURE na KIBULU vyote ni MAKANDE!
Mweh! :-) MAKANDE, PURE AU KIBULU ni mchanganyo wa mahindi na maharage nk au?
Post a Comment