Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SHERIA kama zinatungwa na BINADAMU na atungae ni MBUNGE msenge KIFISADI,...

>> Thursday, May 19, 2011

.....usenge unaweza usiwe  kisheria ni kosa la jinai hata kama  JAMII inafikiria ni DHAMBI!:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri nani ni MJINGA mpaka atunge SHERIA zimbanazo yeye MWENYEWE kiulaji wakati unajua moja ya sifa za BINADAMU ni kupenda kula kiulaini?


Na SHERIA kama inatungwa  na MWIZI kifisadi,....
..... labda  kitafsiri haiendani na tafsiri za WANANCHI za ni nani ni FISADI,...
.... kitu kiwezacho kufanya KISHERIA labda UFISADI usiwe ni uvunjaji wa SHERIA  hata kama kuna waaminio UFISADI mbele za muumba ni DHAMBI!:-(

Swali:
  • SI unajua SHERIA hutungwa na BINADAMU na BINADAMU moja ya sifa yake kuu ni UDHAIFU?
  • Na  si inajulikana  SHERIA  inahitaji TAFSIRI ili ibane mtu na kama SHERIA zitungwazo na MWIZI kitafsiri WIZI ujulikanao katika jamii haiutambui sikuna uwezekano KISHERIA mwizi sio MWIZI?


Na kwa kuwa SHERIA na HAKI ni vitu viwili tofauti,...
......kama SHERIA ikitungwa na MWIZI,....
...... kisheria wizi huweza kuanzia kwenye UJAMBAZI ,...
.... kitu kifanyacho wewe kama ni MDOKOZI au tu MWIZI na hujafikia bado UJAMBAZI ,...
.... kisheria LABDA wewe unafaa kutunukiwa Utakatifu na Kanisa la Roma  kwa kuwa MTU SAFI hata kama kiukweli huna hiyo HAKI!:-(

Swali:
  • Si unajua NAWAZA tu hapa KIJIWENI MHESHIMIWA?
Ndio,...
.... na kama SHERIA ni msumeno,....
..... basi KIFISADI labda sheria haiwakati sana wenyenazo ,....
...ukizingatia KISHERIA ni walalahoi ambao hawashindi KESI hata kama HAKI ni yao!:-(


NI hilo tu!:-(


Hebu twende Brazil ili Sergio Mendes atekenye tena -Magalenha



Sergio Mendes adinye tena na- funky bahia



Kabla Sergio Mendes hajadinya tu  akiwa na Black Eyed Peas ndude -Mas Que Nada


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:25 pm  

Sasa hapa sijui tunaweza kusema binadamu huyu ni mjinga/mpumbavu atungaye sheria au? maana anatunga sheria anamtungia nani? kwani yeye si Binadamu?...najaribu kuwaza tu kwa sauti....UDANGANYIFU!!!

emu-three 12:42 pm  

Mkuu kwa ufupi sheri ani msumeno, haujalishi umetunga wewe au nani unapenda au hupendi....mmmh, au sio mkuu!

Simon Kitururu 1:31 pm  

@Mrembo Yasinta: Mmmmh!

@M3:SI nasikia SHERIA kwa MAFISADI mbele za watunga sheria na wasimamia sheria MAFISADI msumeno huwa butu kwa MAFISADI?

Yasinta Ngonyani 2:15 pm  

Mmmmmhhh! kaaaazi kwelikweli!!

Goodman Manyanya Phiri 3:54 am  

Demokrasia inayo lugha moja tu: Akina nani ndiyo wengi?

Sasa, kwa mujibu wa
http://news.bbc.co.uk/2/hi/americas/4237171.stm

ni kasorobo tu yasisi binadamu wenye tabia au maumbile ya kisenge. Kwa hiyo hata huko bungeni msenge na wasenge wenzake watashindwa tu. (TUWAPATAPATEJE WATOTO, MKUU, TUKIWA SOTE TUNA ITIKIA SHERIA ZA KISENGE?)

Shaaban Fundi 4:40 am  

Mmmh! Demokrasia ama domolawazee? sijui lipi ni jipi? Kwani ukiwachia fisi kutunga sheria si watatunga sheria ya kuwalinda wao? Mafisadi watungapo sheria huzingatia ufisadi katika sheria wazitungazo. Ndio maana mvuta bangi anafungwa miaka mitano na viboko dazeni wakati mwizi wa benki kuu au mmiminaji wa mali ya uma anaachiwa huru mahakani.

Simon Kitururu 5:24 am  

@Mkuu Goodman: Na mie sijawahi kuona katika DEMOKRASIA yoyote ile kuwa ni wengi walioshinda!:-(
Vigezo vyangu ni :
Kama MArekani wale wapendao kusakizia wengine DEMOKRASIA nafikiri unakumbuka juzijuzi AL GORE ndiye alikuwa na kura za watu wengi lakini MSHINDI alikuwa George BUSH kwa kuwa watakuambia kuwa kihesabu zao kiuzito wa STATE au KOLEJI auchochote watakachodai ndio mwenye kura za watu wachache ndiye mshindi.

Pili mie siamini hata kwa mfano TANZANIA ambako asilimia ya watu kibao wanaweza kukupigia kura kisa umegawa kanga na ubwabwa kwa hiyo kwakuwa wachache wajuao ni kweli ungebadili nchi ki chanya maana yake kwa kuwa wengi hawakuelewi maana yake ndio umeshindwa!:-(

Mie namuelewa Gadafi na Saddam Huseinn kiani mara nyingi kuliko NATO na waaminio katika maelfu zaidi ya wafao tokea Saddam Husein auawe na ilipoanzishwa vita na wana demokrasia ili kuleta demokrasia Libya saaa nyingine!

Na sibishi ,...
labda huko BUNGENI msenge na wasenge wenzake watashindwa tu ,...
... lakini kabla hawajashindwa chamoto tunakiona!:-(


@Shaaban Fundi:Yani umegusa palepale kwenye maumivu na hata sina cha kuongezea!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP