Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Siri za watu kujifungia MLANGO chooni ihatarishwavyo na Macho, MASIKIO, pua, ngozi katika mpapaso na ULIMI!

>> Sunday, May 08, 2011

Macho, MASIKIO, pua, ngozi katika mpapaso na ULIMI,...
... ndivyo vihatarishavyo SIRI za watu! 





Swali:
  • SI umestukia eeh?

Ndio,...

....ingawa vifanyikavyo hata  MSALANI  hudhaniwa ni  siri kwa kuwa HUNUSWA ila havionwi,...

... labda  bado KUJIFUNGIA mlango MSALANI  ni moja ya kitu kisaidiacho KUTUNZA siri KISAIKOLOJIA tu kwa kuwa kitendo chenyewe cha kujifungia labda hutoa fununu ni nini kinaendelea MSALANI!:-(

Swali:
  • Si labda  KUNAUWEZEKANO nisemacho ni kweli?

Na kama tunajifunza  SIFA za SIRI  kutokana na KITENDO cha  watu kujifungia msalani wakati wanaburudika na FARAGHA ni kwamba,...
.... siri ni KAMA yatendekayo CHOONI kwa kuwa hayo wala sio siri,....
... na kiyageuzayo YAJULIKANAYO kutendeka MSALANI kuwa SIRI ni ukosaji tu VIPENGELE fulanifulani KI-DETAILS aka KI -ABC za undani wa shughuli  kiushuhuda kuwa  ingawa inajualikana MHESHIMIWA alitawadha,...
.... ila alichambaje /alitawadhaje kwa kuwa HAIJULIKANI  ndio huweza kugeuza kitendo kizima CHENYE VIPENGELE VINGI AMBAVYO SIO SIRI kuwa SIRI,...
....hata kama   kitendo chenyewe cha  KUCHAMBA  / kutawadha kilichofanyika  kinajulikana vipengele vyake hatua kwa hatua !:-(



Na ndio,...
.... labda hakuna kifanyikacho DUNIANI ambacho ni SIRI,...
.... ingawa  kifanyacho BAADHI ya VITU kudhaniwa ni siri,...
....ni udhaifu tu wa watu katika kutambua hasahasa  VISIVYO shuhudiwa kwa MACHO yao, PUA, ulimi kupapaswa kimguso  au na MASIKIO yao  !:-(



Swali:
  • SI  kuna siri PIA kutokana na ni jinsi gani TU  ugeuzavyo  VITENDO VIJULIKANAVYO VINATENDEKA kuwa ni SIRI?

Na labda ni KWELI kuwa,...
... siri sio siri mpaka mtu awe na hamu ya hicho kitu asichokijua  KUKIJUA!





NI wazo tu hili DHAIFU Mkuu!
Jumapili njema MHESHIMIWA!

Hebu Lil' bits aingilie kati kwa  - Bump



Lil' Bits na Olatunji wadinye- Hold me/Dis Year



Lil' Bits na Sean Caruth wahandisi - Crush on You




Au tu Bomani amalizie kwa  - ON d' ROAD


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:50 am  

Duh! Jumapili njema na wewe Mtakatifu Simon!

Simon Kitururu 9:01 am  

@Yasinta:Asante kimwana Nangonyani !

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP