Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa unaweza kumkata kauli MLEVI kwa kumuita MLEVI na MMAREKANI MWEUSI kwa kumuita MUAFRIKA!:-(

>> Friday, May 13, 2011

Lugha fulanifulani  kwa makusudi huweza kutumika kukata mtu KAULI ,....

... na moja ya NJIA ya kumkata MALAYA kauli wakati anahubiri hata neno la MUNGU kutoka moyoni kabisa,....
.... ni kumuita MALAYA wakati yuko katikati ya MAHUBIRI yake kwa kuwa kwa KITENDO hicho utakuwa UNASHAMBULIA ukubalikwaji wa HOJA ZAKE ZA MUNGU kwa kumfanya ajisikie kutokuaminika na waanzao KUMSIKILIZA huku wakichuja UJUMBE WAKE kwa kutumia KUJUA KWAO kuwa ni MALAYA hata kama asemayo haya husiani na UMALAYA na ni ya kweli.


Swali:
  • AU?
Na,....
..... hata kama aliyekuwa KIRUKA NJIA siku hizi si kweli bado ni MALAYA ,...
..... kwa kumuita MALAYA wakati afanyacho sio UMALAYA ,...
....kisaikolojia inaaminika wakati huo bado unamuweka katika hali ambayo inadhaifisha ujumbe wake hasa kwenye jamii ambayo haioanishi MUUZA KIDUDE/mgawa nanihii MALAYA  na MAHUBIRI ya neno la MUNGU!:-(



Swali:
  • SI wakati  aliyewahi kuwa MSHAMBA ambaye ni bomba la mbunifu wa mambo ya ULIMBWENDE  anatoa lekcha ya mitindo bora tu kiubunifu akiitwa MSHAMBA labda pamoja na kuwa bomba lambunifu kifanyikacho hapo ni kumkata tu makali ili kuua UMAKINI na UMAHIRI wake wa MITINDO ambayo ni kweli kabobea?

Na lugha hukata KAULI,...
....na ndio maana moja ya kulainisha UKWELI aongeao MLEVI wenye HEKIMA tu ilikuutia udhaifu  ,...
... kwa ambao hawajalewa hupenda kutumia silaha za sentensi kama:

``UNamsikiliza MLEVI HUYO?´´ au:
``Huyo mlevi achana naye POMBE tu inaongea!´´....
....wakati labda UKWELI wa KITU saa nyingine asiyeogopa kuuongea KAVUKAVU ni yule MLEVI kama una SIKIO!:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Kwani unafikiri UKWELI kama aongeaye KALEWA hubadilika kuwa UONGO?


Ndio,...
.... kuna sababu MLEVI anaweza akavumiliwa kuitwa MNYWA POMBE kuliko MLEVI,...
... hasa kama neno MLEVI anahisi linatumika tu kama kichujio cha kugeuza yake ya HEKIMA kuchukuliwa ni ya KILEVI tu na wale WENYE SIKIO lakini hawasikilizi maneno yasemwayo huku wakiyatafakari  kisa wanaamini kwa kuwa aongeaye ni MLEVI basi iongeayo ni pombe tu hapo.:-(


Swali:
  • Ushawahi kumsikiliza MLEVI au huwa kabla ya kumsikiliza huwa unaamua kuwa KALEWA kwa hiyo hana lakuongea la maana kwa staili ileile ya waaminio kwa kuwa aongeaye ni MHESHIMIWA basi  kila aongeacho si PUMBA zenye harufu ya mtu kajamba?

Ndio,...
... kuna maeneo ukitaka MLOKOLE ajuaye ulimbwende asisikilizwe na wajanja wa kiwanamitindo/WAUZA SURA  wapya kwenye fani,...
.... waweza kumkata kauli kwa kusema:
``MLOKOLE huyo unafikiri anajua nini kuhusu MITINDO ya jinsi ya kunyoa nywelenywele za sehemu za siri ili BIKINI ya KIBRAZILI ing'ae bila bughuza za vichaka vya nywele za asili kuharibu muonekano wa MUUZA SURA  mbele ya majaji kwenye FASHENI SHOO ya mitindo dukinaa ya fulu kuiga Wazungu?´´......
..... na WAINGILIAO VITU kwa pupa na wasiooanisha ULOKOLE na ujuzi wa kupendeza uchi  wanaweza wakaingia  mkenge  kwa sentensi hiyo na KUDHARAU  uwezo wa MLOKOLE kupendeza uchi,...

 .....wakati inawezekana aliyekubuhu katika kurembesha maandalizi ya sehemu za siri ili mtu apendeze bila nguo anaweza akawa ni huyo MLOKOLE ndio bingwa wao kwa kuwa KUOKOKA na kupendeza uchi vinashabihiana tu na wala sio DHAMBI na haki ya nani  hata kwenye BIBLIA hicho kitu hakijagusiwa.:-(

Tukiachana na hilo,...
Swali: 
  • Si unajua watu wengi TANZANIA humkata kauli MKULIMA kwa kumuita MKULIMA ?

Ndio,...
..... kuna wamkatao mpaka MKULIMA kauli TANZANIA kwa kumuita MKULIMA,...
.... kwa kuwa katika matumizi ya LUGHA  kwa kumuita mkulima ; ``MKULIMA´´ .....
....wanamaanisha ni MSHAMBA  kwa hiyo hajui anachoongelea  hata kama aongeleacho ni  tako na haki ya nani tena TAKO hata wakulima wanalo tu vizuri kabisa!:-(

NIMEACHA!
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ijumaa na WIKIENDI NJEMA!



Hebu UB40 walainishe kwa-ADELLA



 UB40 wadinye tu na- Sardonicus


Au tu UB40 warudie tu na - Sing Our Own Song

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP