Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kuna wajambia SEBULENI kama hakuna WAGENI!:-(

>> Sunday, May 22, 2011

Maishani ,...
.... labda kumbuka kuna vitu havifanywi,...
... kwa kuwa TU hapo wewe  UPO,...
.... na kama usingekuwepo  SEBULENI  kuna wastaarabu UDHANIAO KWA SHUGHULI ZA USHUZI ni  waendao chooni AMBAO  hapo SEBULENI  ni kiwanja chao cha kujambia aisee !:-(

Swali:
  • Kwani unafikiria watoto wote wa MSTAARABU mwenye aibu KWAKO walitengenezewa chumbani?


Ndio ,..
....LABDA kumbuka mengi ushuhudiayo WAZIWAZI,...
.... labda kuna watakao USHUHUDIE waziwazi,....
.... na ndio maana  MENGI ya udhaniao unawajua NJE-NDANI ,...
.... kuna mengi hustukii watakayo usistukie  kitu kifanyacho uwaheshimuo labda unaweza kuapia hawajambi kwa kuwa hujawahi kusikia wakijamba kitu ambacho BAOLOJIA inatuambia kuwa BINADAMU yoyote mwenye afya ya kutosha lazima ajambe mara kadhaa ndani ya siku,...
..... na KIBAOLOJIA hatuelezwi kuwa  mwenye afya anahitaji kujificha tusistukie kaachia ushuzi!:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri ni wangapi hushuhudia waheshimiwa wakati wanafanya UFISADI ingawa wanajulikana ni MAFISADI?
  • Na si unakumbuka MDOKOA MBOGA hujulikana ni MDOKOA MBOGA  pale tu akidakwa anadokoa mboga hadharani kitu kifanyacho wadokoa mboga ni kwa asilimia chache sana wanatambulika HADHARANI? 

Ndio,...
... labda kama hakuna WAGENI au UMATI ,...
.... sebule  kama HADHARANI  kote ni nusu choo kwa kuwa nusu ya yafanywayo chooni na MHESHIMIWA huweza kufanyika vyema tu hadharani au  SEBULENI!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA,...
.... na samahani kwa UjingaBUSARA huu kama haujakugusa maeneo!:-(

Hebu FELA KUTI arudie- SHAKARA






Au sijui kwanini hebu DEAD PREZ warudie-Malcom,.. Garvey,... & Huey


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP